SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 25 Agosti 2016

T media news

DESIIGNER AMEPATA MAFANIKO MAKUBWA NA NGOMA YA “PANDA”


Rapper ambaye mpaka sasa mashabiki wake hawamwelei vizuri kwenye staili yake ya uimbaji, namzungumzia Desiigner, Ngoma yake ya Panda imefanikiwa kuuza kopi Milioni 3.
Baada ya ngoma ya “Panda” kuachiwa, ilijizolea umaarufu mkubwa kutoka sehemu mbalimbali Duniani na kufanya ngoma hii kuwa ya kwanza kwenye chati za BIllboard hot 100 kama wimbo wa Hiphop na kufanikiwa kuupindua wimbo wa Wizkhalifa “See you Again” kwenye chati hizo.
Taarifa za Mauzo hayo ya ngoma ya “Panda” zilitolewa kwenye ukurasa wa twitter wa Def Jam recordszikionyesha kwamba wimbo huo umefanikiwa kuuza kopi milioni 3

Kingine kikubwa labda ulikuwa ukifahamu kuhusu ngoma hiyo ni kwamba, imekuwa streamed mala milioni 118 Kwenye YouTube, milioni 122 Kwenye SoundCloud, milioni 380 Kwenye Spotify na video ya wimbo huo imetazamwa milioni 114