Monaco,Ufaransa.
NYOTA wa Real Madrid na Ureno, Cristiano Ronaldo, amechaguliwa kuwa mwanasoka bora wa mwaka wa Ulaya.
Ronaldo mwenye umri wa miaka 31 sasa ametwaa tuzo hiyo usiku huu huko Monaco, Ufaransa akiwashinda wapinzani wake wa karibu Gareth Bale waReal Madrid na Antoine Griezmann wa Atletico Madrid.
Msimu uliopita Ronaldo alifunga mabao 51 katika michezo 48 huku katika michuano ya ligi ya mabingwa akipachika mabao 19 na kuiwezesha Real Madrid kutwaa ubingwa wa 11 wa Ulaya.
Tuzo hiyo ni ya pili kwa Ronaldo mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka 2013-14. Ronaldo na Messi ndiyo wachezaji pekee waliowahi kutwaa tuzo hiyo mara mbili.
Tuzo ya mchezaji bora wa kike wa mwaka imekwenda kwa Mnorway Ada Hegerberg anayechezea klabu ya Olympique Lyon.