...Jeneza la mwalimu John lilikuwa tayari limefunuka, Mwalimu John aliinuka ndani ya Jeneza na kusimama wima cha kwanza alichofanya ilikuwa ni kunyanyua kinywa chake na kumuita mkewe mpenzi kwani ndiye aliyekuwa akimfikiria kila sekunde. " Mke wanguuuuu... Niko hai..usilie" Mwalimu John alisema kwa sauti kuu, huku furaha ikiwa imefurika moyoni mwake kwani hakuamini kama kweli ameurudia uhai.
Akiwa katika furaha hiyo isiyo na kikomo mwalimu John akatahamaki sana baada ya kuona umati wote uliokuwa ukiomboleza kwaajili yake ukikimbia. Watu walikimbia kwa fujo huku hofu ikiwa imewatamalaki. Cha ajabu hata mke wa Mwalimu John pia alikimbia kama swala anayekabiliana na mnyama mkali.
Hakuna aliyesalia kwenye eneo lile, vumbi lilitimka na kuwaaga waombolezaji wote ambao mpaka wakati ule hakuna aliyejua kilichotokea. "Maajabu haya! Maiti kafufuka? Kweli dunia IPO ukingoni" alisikika mwanamume mmoja ambaye alikuwa amejikwaa mguu baada ya kukimbia kwa muda mrefu.Alihema kwa nguvu huku akizitafuta nguvu zingine za kukimbilia. Ghafla akahisi kuna Mtu kasimama nyuma yake
" Vipi kuna mini kwani?" Ilisikika sauti ile ambayo ilipenya vyema masikioni mwa mwanaume yule. Akageuka kutazama anayeuliza, Mwanaume yule alitetemeka sana baada ya kukutana USO kwa uso na Mwalimu John. Akainuka haraka na kuziendeleza mbio zake.
Mwalimu John alikuwa haelewi ni kwanini watu wote wanakimbia, na yeye akaingiwa na hofu akaanza kukimbia akijua labda kuna jambo la hatari linakuja. Alizipiga mbio kuelekea nyumbani kwake ili akajihifadhi haraka iwezekanavyo.
Mwalimu John alipofika mtaani kwao, kila MTU alikimbilia ndani na kujifungia. Ndipo alipozidisha juhudi na kuongeza mwendokasi akidhani hatari inamkaribia. Mwalimu John alifika nyumbani kwake, alipofika getini ghafla geti likafungwa. Akastaajabu sana kwani hakufikiria kuwa mkewe badala ya kumpokea kwa shamrashamra alimfungia mlango.
"Nifungulie mke wangu!" Alisema Mwalimu John huku akipigapiga mlango, na kwakuwa mlango haukufungwa vyema ukajifungua. Mwalimu John aliingia ndani huku akihema sana.
"Mamaaaaa!"
Zilisikika kelele ndani ya nyumba ya Mwalimu John, ndugu wote walipiga kelele.
"mke wangu! Hunitaki!?" Mwalimu John aliuliza kwa sauti ya kutia huruma, huku akimsogelea mkewe.
"Ushindweee!" Mkewe alifoka.
"Mke wangu nishindwe Mimi? Leo unaniambia nishindwe kwani Mimi pepo?" Mwalimu John alizidi kutia huruma.
Aliinamisha kichwa chini, kwa bahati macho yakatua mwilini mwake. Mwalimu John alishtuka kupita kiasi, akajiogopa na akatamani