Cristiano Ronaldo ameshinda kila kitu akiwa mchezaji wa kwenye level ya klabu, yeye binafsi ameshinda tuzo nyingi ikiwemo ya mwanasoka bora wa dunia Ballon d’Or, lakini bado anakiu ya kuiongoza nchi yake ya Ureno kuchukua ubingwa wowote ule.
Hii ndiyo changamoto ambayo pia ilikuwa inamkabili mpinzani wake Lionel Messi ambaye baada ya kuiongoza Argentina kufika fainali ya Copa America na kushindwa kuchukua ubingwa huko nchini Marekani.
Vita kati ya hawa vidume wawili katika kizazi hiki bado inaendelea, Cristiano Ronaldo jana usiku aliiongoza Ureno kutinga fainali ya michuano ya Euro 2016, nini kina fatia baada ya hapo, atafanikiwa kuiongoza Ureno kubeba ubingwa wa Euro? Au ataungana na mpinzani wake Lionel Messi ambaye alishindwa kuiongoza Argentina kutwaa ubingwa wowote?
Baada ya Messi kushindwa kutwaa ubingwa wa Copa America 2016 alitangaza kustaafu soka la kimataifa, Je Ronaldo ataweza kuiongoza Ureno kutwaa ndoo baada ya kufuzu kucheza fainali au na yeye akipigwa kwenye mchezo wa fainali atafuata nyayo za mpinzani wake Lionel Messi kuachana na timu ya taifa?
Hilo ndiyo swali au kitendawili kilichobaki sasa kinachosubiri kuteguliwa.
Nusu fainali nyingine inayosubiriwa kwa hamu ni kati ya wenyeji wa mashindano Ufaransa dhidi ya Ujerumani mechi itakayopigwa ni mchezo ambao wafaransa wanausubi kwa hamu kubwa.