Staa wa Bongo Fleva, Omary Nyembo ‘Dimpoz’ na Zee.
Stori: Boniphace Ngumije, Risasi jumamosi
DAR ES SALAAM: Jambo limezua jambo! Baada ya kuvuja kwa picha zake akiwa na Mwigizaji Wema Sepetu ‘Madam’ kitandani, mchumba wa staa wa Bongo Fleva, Omary Nyembo ‘Dimpoz’ anayependa atajwe kwa jina moja la Zee, amegombana na staa huyo.
Chanzo makini kilicho karibu na Dimpoz kimeeleza kuwa, mara baada ya habari hiyo kuchapishwa na gazeti hili, Jumamosi iliyopita, penzi la Dimpoz na Zee lilimeguka na hadi sasa hawana mawasiliano mazuri.
Dimpoz na Wema.
“Yaani gazeti lilipotoka tu, mtoto wa kike kaja juu, amemaindi kwelikweli. Dimpoz kajaribu kumuelewesha kwa kumwambia ni picha za kitambo lakini wapi. Mtoto wa kike kakaza balaa, hivi sasa hawazungumzi kabisa,” kilisema chanzo hicho.
Mara baada ya ubuyu huo kutua gazetini mwanahabari wetu alimvutia waya Dimpoz, alipopatikana alikiri kutokea kwa ugomvi na mpenzi wake kufuatia kuvuja kwa picha zake na Wema lakini akadai atayaweka sawa mambo.
“Yeah ndiyo hivyo bwana, kimenuka kwelikweli lakini naamini yatakwisha si unajua tena picha zenyewe ziliibwa kwenye simu yangu na ni za zamani, najaribu kuzungumza naye naamini atanielewa,” alisema Dimpoz.