Ukitaka kujua umaskini ni nini, inabidi kwanza ujue kutokuwa maskini ni nini? Uwezo wa kumudu maisha ya chini kabisa (yaani kupata chakula kizuri, malazi mazuri, elimu, mavazi na usafiri mzuri na wa hakika), kuwa na uhakika wa kupata matibabu mazuri unapoumwa, uwe na uhakika wa kupata mapumziko na burudani baada ya kazi, uwe na uhakika wa maisha yako na kupata mahitaji hayo kwa walau miezi mitatu. Hapo unaweza kusema kuwa wewe sio maskini. Kama huwezi kupata hayo basi upo kwenye kundi la maskini kama mimi au unakaribia kwenye kundi la maskini.
Lakini kuna wengine wana-definition tofauti ya maendeleo, kwa na wanawake wengi, kunywa pombe na kula nyama mpaka utoke jasho, kuwa na gari la kisasa huku huna hata pa kulala, kuvaa nguo tofauti kila siku na cheni kubwa ya dhahabu, sasa inategemeana na uwezo wako wa kufikiri. Unaweza kuwa maskini na ukajiona si maskini kutokana na unavyofikiri na unaweza kuwa si maskini lakini ukajiona maskini kutokana na unavyofikiri.
CAR FOR SALE: 2000 Toyota Land Cruiser VX 100 Diesel 35m
M
Mwanafalsafa
Senior Member
#3 Oct 8, 2007
Nikitaka kuulezea umaskini vema nitaelezea pesa ni nini kwanza. Pesa ni ubunifu wowote unaosimamiwa na kujiamini kwako. Unapokuwa na wazo zuri la kibiashara au la maendeleo na unapokuwa na confidence ya kulitekeleza kama inavyotakiwa then wewe una pesa. Wewe ni tajiri. Kinyume cha hapo wewe ni maskini.
CAR FOR SALE: BMW 3 Series 318i 2005 Engine 1900cc Silver 12.5m
Gigo
JF-Expert Member
#4 Oct 10, 2007
Wewe Mswahili..Hufikirii Kwamba-Unaweza Ukawa na fedha Kiasi furani lakini bado ukawa masikini!!...Kuna tofauti gani kati ya Tajiri wa mtaa wetu na mtaa wa jirani?
Kalimanzira
JF-Expert Member
#5 Oct 11, 2007
Nakubaliana na wazo kuwa 'umaskini wa mtu unatokana na kiwango anachoweza kufikiri juu ya mahitaji yake na kuyatimiza'. Mtu anaweza kuwa na hela nyingi lakini akajikuta ni maskini ukilinganisha na mahitaji yake, hali kadhalika mtu anaweza kuwa hana fedha, lakini akawa tajiri kulingana na mahitaji aliyonayo kwa wakati huo. Kumbe umnaskini ni 'subjective'siyo 'objective'. Ndiyo maana tajiri wa kijijini kwetu au mtaani kwetu, ni maskini wa kijiji au mtaa mwingine kwa tafsiri na muonekano wake!
Richard
JF-Expert Member
#6 Oct 11, 2007
Mimi ntaelezea jinsi nnavofahamu umaskini.
Umaskini ni ule kwamba huna mahala pazuri pa kuishi (nyumba) nzuri yenye umeme,maji na choo kitumiacho maji, mlo wa mara tatu-asubuhi ,mchana na jioni.
Pia umaskini ni pale ambapo baada ya kutumia pesa ya ujira ulioipata kihalali kwa kulipia labda umeme,maji, na manunuzi ya chakula, unakuwa huna uwezo wa kununua vitu muhimu kama mavazi na masuala yote yahusianayo na utanashati na urembo na mengine ambayo kwa shingo upande tunasema ni anasa.
Pia umaskini ni pale ambapo sasa ndio unashindwa hata kumsomesha mtoto shule kwa kumlipia ada tangu aanze shule ya awali mpaka aingie chuo kikuu na awe na uhakika wa ajira.
Mwisho umaskini ni pale unaposhindwa kushiriki katika mambo mbalimbali ya kijamii na kujiona umetengwa kama kushiriki katika jambo forums na kukosa habari muhimu zinazoendelea mahala unapoishi kama ni Buzwagi na nje ya Buzwagi mpaka Dar-es-Salaam na nje ya mipaka ya nchi yako na kuona habari za kimataifa na kujifunza na kuwa na upeo na uelewa wa masuala mbalimbali yawe ya kiuchumi,kisiasa na kijamii.
Baada ya kuelezea umaskini ni budi kuangalia chanzo chake.
Ukiachailia mbali sababu kama za kiasili za hali ya hewa na mazingira au labda za kijiografia ambapo hapa pana vitu kama ardhi, madini, na mali asilia zingine, umaskini unasababishwa na watu waliochaguliwa katika jamii na kupewa thamana ya kuongoza.
Kwa sababu ukiangalia jiographia na nikitoa mfano wan nchi yetu Tanzania,sehemu kubwa ya ardhi ni yenye rutuba kubwa tu na maji huwa yapo ukiondoa vipindi vichache vya ukame ukifananisha na Darful ambako hakuna uhakika mvua itanyesha lini.
Kwa hiyo hapa serikali imeshindwa kuondoa umaskini kwa kukosa mipango madhubuti ya kumuendeleza mkulima wa mazao ya biashara kama kahawa, chai n