SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 21 Mei 2016

T media news

MICHEZO Man United wamefanikiwa kutwaa taji la FA na kuifikia rekodi hii ya Arsenal

Baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu Uingereza msimu wa 2015/2016, mashabiki wa soka Uingereza walikuwa wanasubiri mchezo wa fainali ya Kombe la FA ambao umechezwa leo May 21 2061 katika uwanja wa Wembley, Man United ambao walikuwa na msimu mbaya walicheza dhidi ya Crystal Palace katika fainali hiyo.

Mashabiki wa Man United walikuwa na matumaini ya kuona Man United ikifanikiwa kutwaa taji hilo hili kujipoza na majonzi ya kukosa nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, lakini kutaka kuona klabu yao ikifikia rekdo ya Arsenal ya kutwa taji hilo mara 12 na kuwa klabu inayoongoza kwa kushinda taji hilo mara nyingi zaidi.

Mchezo ulianza na klabu ya Crystal Palace kupata nafasi ya kufunga goli la uongozi dakika ya 78 kupitia kwa Jason Puncheon, goli ambao lilidumu kwa dakika tatu kabla ya Juan Mata kuisawazishia Man United, dakika 30 za nyongeza ndio zilizoamua nani atwae taji hilo kwani, dakika ya 110  Jesse Lingard akaipatia goli la ushindi Man United.