CEO wa kampuni ya KWL Management inayowasimamia wasanii wakubwa wa Marekani wakiwemo Trey Songz na Big Sean, Kevin Liles, amefunguka kwenye Twitter kuhusiana na ukaribu alionao na Diamond.
Kupitia session yake ya #AskKevinLiles, mtanzania aitwaye Sammy Gratian alimuuliza: Is Tanzanian artist, Diamond Platnumz under your management or possibly working with any artist under your management? #AskKevinLiles.”
Kevin alijibu kwa kupost video akielezea kuwa yupo karibu na Diamond kama washkaji.
“Shout outs to my friend Diamond Platnumz and my whole Tanzania crew,” anasema Kevin kwenye video hiyo.
