SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 25 Mei 2016

T media news

MAMBO MATANO NILIYOJIFUNZA UEFA CHAMPIONS LEAGUE KUELEKEA SAN SIRO

Na Brian Marian Mrope(Gascoigne Brian)

Diego Simeone mmoja kati ya viumbe wachache sana dunianiambao wanaweza kuwahi kuuona ufalme wa mbingu kwa hikianachotupa. Anajua sana kucheza na wakati wa mwanadamu hasa linapokuja suala la (Knockout stage) hatua za mtoano. Mshairi mmoja nchini uingereza aliwahi kusema Bora saa tatu mapema mno kuliko dakika kuchelewa mno. Huyu wa juu achana na vurugu zake pembezoni mwa uwanja jaribu kuuona ubunifu na ubora anaotupa kila mwishoni mwa msimu ni ubora ulioje!

Hata safari yake ya kuelekea San Siro haikuwa rahisi, aliweza kupanda na Alteza katika milima ya Uluguru na akafanikiwa katika safari yake ya kuelekea San Siro. Ni wanadamu wachache sana wanaoweza kufanikiwa katika hili. Hasa tukiangalia na ubora wa kikosi chake, kilichojaa ubunifu ndani yake ni wakati wa kupumzika
zako Ibiza ukisubiri kuthibitisha ubora wako pale San Siro.

Zinedine Zidane haikuwa rahisi kuweza kuamini ulichonacho, taratibu unaanza kubaki ndani yetu. Kwa kipindi kifupi ulichoweza kukaa na timu umebadili kila kitu hakika unastahili pongezi juu yahili. Bado naiwaza kesho iliyo bora kwako hasa kwa hiki unachozidi kutupa, naiwaza sana hii fainali hakika itakuwa na mambo mengi yakuelezeka hasa tukijaribu kuangalia ubora wa makocha wenyewe. Zinedine Zidane sijui utatupa kilicho bora au kitachostahili ndani ya ubongo wako! Wacha niendelee kusubili utamu wa pambano hili litakalojaa ubabe ndani yake huku utulivu wa S. Ramos ukihitajika sana katika mchezo huu, huku ubunifu wa L. Modric ukihitajika ndani ya miguu yake pia. Namwona Florentino Perez pembezoni mwa fukwe za Otranto nchini Italy akiwa amepumzika na mkewe kipenzi akisubiri utamu wa C. Ronaldo uweze kumletea thamani ndani ya klabu yake.Pep Guardiola kiumbe mwingine aliyejaribu kutupa kila kitu katika soka, ndiye aliyeweza kurudisha lile soka la Tiki Taka tulilokuwatumeshalitupa katika uso wa dunia yetu. Ubora, mbinu, ubunifu ndiyo silaha yake ya siku zote katikati ya uwanja. Anakupa unachotakakupitia ubongo wake uliojaa ubunifu ndani yake. Ameweza kushinda karibu kila kitu katika ngazi ya klabu. Wakati na dakika alijaribu kukimbizana navyo pale Alinz Arena tatizo aliweza kufanikiwa katika dakika. Wakati alishindwa kukimbizana nao kwakuwa hakuwa na Messi mwingine pale Alianz Arena, hakuwa na Iniesta mwingine pale Arena wala hakuwa na Xavi mwingine pale
Arena.

Wakati mwingine ubora wa kiumbe hapa duniani hubebwa na ubora wa watu waliomzunguka. Mahala pa Messi pale Arena yupo Coman, mahala pa Iniesta yupo Alcantara, mahala pa Xavi yupo Vidal. Nafikiri hapa ndipo mahali ambapo aliposhindwa kuwa karibu na wakati na matokeo yake akawa karibu na dakika. Bado wajerumani watalia na yeye kwa kushindwa kuwapa UEFA Champions League kupitia timu yao. Waliamini sana ubora wake kupitia ubongo wake uliokuwa unamwaminisha kuwa kucheza soka la pasi ndiyo silaha yake ya ushindi. Karibu katika ligi ya EPL iliyojaa kila aina ya ladha ndani yake.

Manuel Pellegrini ahsante kwa zawadi hii uliyowapa Manchster City hakika utaingia hadi katika vitabu vya kumbukumbu vyaManchester City. Tatizo walikutoa uhai mapema wakati bado unaishi. Waliamini ubongo wako umeishia pale,hawakuamini kuwa unaweza kumpa Aguero virutubisho vilivyo bora vya kuweza kuendelea kuwa bora katika EPL. Ila ubora wako utaendelea kubaki ndani yetu siku zote. Kivuli chako bado kitaendelea kuwepo ndani yao, historia ya klabu yako katika michuano ya Ulaya ndiyo yamekuhukumu.

Ulikuwa na kikosi bora katika michuano hiyo tatizo mzimu wa Billy Shanky ndiyo umekunyima nafasi. Wakati mwingine pesa siyo kila kitu katika maisha ya mwanadamu. Muulize Vichai Srivaddhanaprabha bosi wa Leichester City atakwambia kuhusu hili. Pole sana Pellegrini kwakushindwa kuwapeleka Manchester City San Siro Ila wakati utatuambia tu thamani ya ubora wako ulivyowapa Manchester City.Ni kipindi ambacho unatakiwa ukapumzike na mkeo mwanamama Carola Pucci pembezoni mwa Punta Arenas huku Chile ukipumzika na familia yako kazi yako ya Etihad wameimaliza mapema imani yangu bado ulikuwa una kitu cha ziada.

Ndiyo mahala ambapo makocha wote walihitaji kwenda pale, tatizo ubora na utimamu wa vilabu ndiyo kumewafanya wengine wameshindwa kufika hapo. San Siro ni moja kati ya viwanja vyenye heshima kubwa sana katika ngazi ya klabu. Haikuwa rahisi kwa vilabu kufika pale ilihitaji ubunifu sana kwa makocha hawa kuweza kuwapeleka wachezaji wao mahala pale. Wacha nisubiri ubora wa safari ya hawa watu wawili wanaotoka katika jiji moja. Hakika itakuwa moja kati ya mechi zitakazowavutia kila shabiki wa soka pembezoni mwa uso wa  dunia. Hasa tukiangalia ubora wa vilabu vyenyewe. Atakae kuwa bora katika mchezo huu ndio mwenye nafasi kubwa ya kupata ushindi. Ni mechi itakayojaa ubabe ndani yake, huku mmoja akihitaji kulipa kisasi huyu mwingine akihitaji kuendeleza ufalme wake katika michuano ya Ulaya.