SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 6 Aprili 2016

T media news

MAUMIVU WAKATI WA KUKOJOA

Maumivu Wakati Wa Kukojoa


Maumivu wakati wa kukojaoa ni hali inayotokea kwa watu wengi ikisababishwa na magonjwa mbalimbali. Maumivu wakati wa kukojoa hujulikana kwa kitaalamu kama dysuria. Kati ya sababu kuu za maumivu wakati wa kukojoa ni maambukizi ya mfumo wa mkojo(Urinary tract Infection – UTI) hasa kwa wanawake na magonjwa ya zinaa.
Namna Maumivu Wakati Wa Kukojoa Yanavyotokea

Maumivu haya hutokana na kuchubuka kwa njia ya mkojo. Maumivu huwa yanakuwa ya kuungua wakati mkojo unatoka. Yanaweza kuwa wakati wote unakojoa, mwanzoni au mwishoni mwa kukojoa.
Pia yanaweza kuambatana na dalili kama homa, kuokwa na usaha au uchafu sehemu za siri, kutokwa mkojo wenye damu damu na maumivu chini ya kitovu.
Maumivu haya hutegemea na chanzo cha ugonjwa unaoleta dalili hii. Baadhi ya sababu za maumivu wakati wa kukojoa ni:
Maambukizi ya Njia ya Mkojo (Urinary Tract Infection – UTI)

Ugonjwa huu huleta maumivu kama ya kuungua kwenye njia ya mokojo. Pia maumivu yanaweza kufika mpaka chini ya kitovu wakati wa kukojoa. Dalili nyingine zinazoweza kuambatana na hali hii ni homa, kukojoa mara kwa mara, kuhisi mkojo hauishi kwenye kibofu na maumivu ya mgongo.
Magonjwa ya Zinaa

Huleta maumivu wakati wa kukojoa hasa kwa wanaume, maumivu kama ya kuungua wakati mkojo unatoka. Dalili nyingine zinazoweza kuambatana na magonjwa haya ni kutoa uchafu kama usaha sehemu za siri, maumivu chini ya kitovu na homa.
Kichocho

Kichocho husababisha maumivu wakati wa kukojoa ikiambatana na kutoa mkojo wenye damu.
Magonjwa mengine yanayoweza kusababisha maumivu wakati wa kukojoa ni:
  • Saratani ya kibofu cha mkojo
  • Mawe ya figo
  • Kuumia wakati kufanya mapenzi

Vipimo

Vipimo vifuatavyo vinaweza kufanyika ili kujua chanzo cha maumivu wakati wa kukojoa.
  • Kipimo cha uchunguzi wa mkojo (urinalysis)
  • Kuotesha mkojo (urine culture)
  • Kipimo cha Ultrasound ya tumbo na kiuno (Pelvic and abdominal ultrasound)

Matibabu

Maumivu wakati wa kukojoa ni dalili, hivyo matibabau huelekezwa kwa ugonjwa unaoleta tatizo hili. Maumivu haya yanaweza kutibiwa na kupona kabisa. Ikiwa mtu atapata tena maambukizi yaliyoleta dalili hii awali, basi maumivu haya yanaweza kujirudia tena.