AMINI NYAUNGO
Miaka ya hivi karibuni wapenzi wa michezo haswa ligi ya Hispania walikuwa wakilalamika ligi hiyo kuwa ya timu mbili na zikibaki mechi tano bingwa kashajulikana. Mwaka huu imekuwa tofauti kidogo kwani hajulikani nani bingwa kizuri zaidi uhasama umehamia katika magoli.
MAGOLI YAKOJE?
Vita hiyo bado inatawalia na Rael Madrid na Barcelona, hapo awali ilikuwa ya Messi na Ronaldo mwaka huu imekuwa ya wote haswa Ronaldo na Suarez,Cristiano Ronaldo ana magoli 31 wakati Luis Suarez ana magoli 34.
MATOKEO
Real Madrid ndio walianza kuichabanga Rayo Vallecano 3-2 Ronaldo hakucheza kutokana na majeruhi katoa mwanya kwa Luis Suarez kawasha taa nyekundu baada ya kujipatia magoli 4 katika ushindi wa magolo 6 ya Barcelona.
LIGI IKO WAPI SASA
Kwa mahesabu yalivyo kama wakifungana alama Barcelona Bingwa lakini kilochopo kwa sasa atakae fungwa katika mechi zinazofuata ndio atakuwa ametolewa katika harakati za ubingwa wa ligi hiyo. ambapo mechi zilizo baki 3 ili ligi iishe.