SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 18 Machi 2016

T media news

Standard Bank na IPTL kulipa madeni ya walimu

Serikali imetakiwa kutumia fedha za Standard Bank dola milion 600 pamoja na fedha za IPTL kwa ajili ya kuwalipa walimu madeni yao mbalimbali ambayo yanakadiriwa kufikia shilingi bilioni 480 ikiwa ni stahiki zao mbalimbali wanazoidai serikali.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Maendeleo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge Mh. Raphael Chegeni ambaye pia ni Mbunge wa Busega kwenye kikao kilichowakutanisha wajumbe wa kamati hiyo, Wadau wa Elimu na Wizara ya Elimu kwa lengo la kujadili changamoto za elimu na kuzipatia muongozo ambao utaweza kuwasaidia walimu na sekta mbalimbali kutoka kwenye migogoro ya madeni na serikali.

Mh. Chegeni amesema suala la kimahakama na kisheria likikamilika kiuchunguzi basi fedha hizo zitumike kusaida kulipa madeni ya walimu, kuboresha sekta ya afya na kuboresha maisha ya watanzania wote na kamati yake itahakikisha fedha hizo zinarudishwa kwa watanzania bila ubaguzi.

Kwa upande wake Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amesema pendekezo hilo la Kamati ya Bunge atalichukua na kulipeleka katika ngazi ya juu ya Rais ili liweze kutolewa maamuzi.

Vilevile Prof. Ndalichako amesema serikali katika kutekeleza mpango wake wa Matokeo Makubwa Sasa wameanza kukarabati shule na taasisi kongwe 88 za elimu ambazo zimeharibika na zoezi hilo ni kwa mikoa yote ya Tanzania Bara na visiwani.