SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 18 Novemba 2017

T media news

RC MAKONDA KUPOKEA MELI KUBWA YA JESHI LA CHINA YENYE HOSPITAL NDANI


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa *PAUL MAKONDA* anataraji kupokea *Meli kubwa ya kisasa kutoka Nchini China* inayowasili Nchini *November 19* kwaajili kutoa huduma za *upimaji na Matibabu ya Magonjwa yote Bure* kwa Wakazi wa Dar es Salaam kwa muda wa *Siku Saba.*

Meli hiyo kubwa ya aina yake ya *Jeshi la Maji la China* itawasili Bandari ya Dar es Salaam ikiwa na *Madaktari Bingwa na Wataalamu wa Afya zaidi ya 380* ina uwezo wa kufanya *upasuaji mkubwa na mdogo* ndani ya meli kwa zaidi ya *Watu 600 kwa siku.*

*RC MAKONDA* amewatangazia wananchi *kuchangamkia fursa* hiyo ya huduma ya matibabu bila malipo kuanzia *November 20 -25 ndani ya Meli.*

*MAKONDA* amesema Meli hiyo itatoa matibabu kwa *Magonjwa ya Figo, Saratani, Ini,  Moyo, Macho, Sukari, Presha* ambapo watakaopimwa na kugundulika kuwa na tatizo *watapatiwa Dawa na matibabu Bure.*

Aidha *MAKONDA* amesema huduma hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa *kuokoa gharama za matibabu kwa Wananchi* ikiwemo ile ya *kusafirisha wagonjwa nje ya nchi* kwakuwa ndani ya meli zitapatikana huduma zote ambazo hazipatikani kwenye hospital za Tanzania.

Hatua hiyo ni *utekelezaji wa ahadi iliyotolewa na aliekuwa Balozi wa China  Nchini Tanzania* aliyoitoa wakati wa *Zoezi la upimaji wa Afya bure* ambapo aliahidi kumuunga mkono *RC MAKONDA* katika kuboresha Sekta ya Afya.

Jambo jingine litakalifanywa na wataalamu hao ni *kukarabati vifaa vyote vya hospital za Dar es salaam*vitakavyokuwa na matatizo ikiwemo Ultrasound na Xray ili ziweze kufanyakazi upya ambapo pia *madaktari hao watakuwa wakibadilishana uzoefu na utaalamu na madaktari wa Tanzania.*

Mbali na hilo Madaktari hao watatembelea *vituo vya kulelea watoto yatima* kujionea namna serikali inahudumia watu Hawa wa kundi maalumu pamoja na siku ya moja ya *kubadilishana  utamaduni wa mavazi,  vyakula na michezo*.

*RC MAKONDA* amemwambia Mganga Mkuu wa Mkoa *kuwaita Wagonjwa wote waliokuwa wamepangiwa kufanyiwa upasuaji tarehe za mbali kutokana na ufinyu wa huduma kupelekwa kufanyiwa huduma Bure.*

Nae Kamanda wa Jeshi la Maji la China *Meja Xing Song* amesema zoezi hilo ni matunda ya ushiririkiano wa kidiplomasia baina ya Tanzania na China ambapo wamesema watazidi kushirikiana na *RC MAKONDA*