SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 18 Novemba 2017

T media news

Aliyetajwa kufariki katika ajali ya ndege Ngorongoro anusurika

Mfanyakazi wa hoteli za kitalii za andBeyond Serengeti, Moses Muhina aliyetajwa kuwa ni miongoni mwa abiria waliofariki dunia katika ajali ya ndege ya shirika la Coastal Aviation, imebainika alibadili ndege muda mfupi kabla ya safari ili kuwahi kazini.

Muhina ambaye ni mwongozaji watalii katika hoteli hiyo, alikuwa aondoke na ndege ya Coastal Aviation saa nne asubuhi lakini viongozi wa hoteli walimbadilishia ndege, hivyo aliondoka na Air Exel iliyofika salama Serengeti.

Meneja Uendeshaji wa hoteli ya andBeyond Serengeti UnderCanvas, Mussa Matala alisema kuwa Muhina ambaye jina lake linasomeka Maina,  kwenye orodha ya abiria waliokuwamo ndani ya ndege ya Coastal Avoation, alikuwa apande ndege hiyo lakini waliamua kumbadilishia ili awahi kazini.

Musa Matala alisema kuwa waliomba jina lake liondolewe kwenye orodha ya wasafiri wa ndege hiyo lakini kwa bahati mbaya hadi ndege ilipoondoka jina lake lilikuwepo.