Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi Onesmo Lyanga amesema kuwa watu wawili wamepigwa risasi katika kijiji cha Nyamisati wilayani Kibiti mkoani Pwani usiku wa kuamkia leo na kisha waliofanya tukio hilo kuwachukua majeruhi na kuondoka nao pasipojulikana.
Ametoa kauli hiyo baada ya kuwepo kwa taarifa za awali zisizo rasmi kutoka kwa watu ambao ni wakazi wa kijijini hapo waliodai kushuhudia tukio hilo na kusema kuwa watu watatu waliuawa.
Kamanda Lyanga alitoa ufafanuzi huo na kusema kuwa wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ikiwa ni pamoja na kufanya jitihada za kuwapata majeruhi hao haraka iwezekanavyo.