SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumapili, 22 Januari 2017

T media news

Simiyu Yapania Kuongoza Mapinduzi Ya Kilimo Cha Umwagiliaji Nchini

 Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mataka na ujumbe wake katika mazungumzo na Bw.  Seif Ahmed, afisa mkuu wa NMB upande wa biashara ya kilimo (Agribusiness) na timu yake makao makuu ya Benki hiyo  mwishoni mwa wiki jijini Dar es salam

Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mataka na ujumbe wake katika mazungumzo na Bw.  Seif Ahmed, afisa mkuu wa NMB upande wa biashara ya kilimo (Agribusiness) na timu yake makao makuu ya Benki hiyo  mwishoni mwa wiki jijini Dar es salam.

BENKI ya NMB imekubali kutoa fedha kwa ajili ya kujenga 'skimu' kubwa ya mfano ya umwagiliaji katika Wilaya ya Busega mkoani Simiyu.

"Maji ni raslimali muhimu sana inayotoa uhakika wa kuvuna pamoja mbali ya pembejeo na uhifadhi', alisema Seif Ahmed, afisa mkuu upande wa biashara ya kilimo (Agribusiness) mwishoni mwa wiki.

"Mkuu wa Mkoa ninakupongeza wewe na timu yako kwa nia ya kuwaletea wananchi wa Simiyu maendeleo, " alisema na kuongeza, "Ninawahakikishia kuwa tutawapatia mkopo huo."

Ahmed aliahidi kufanya kazi pamoja na Mkoa wa Simiyu kuhakikisha mradi unaleta mabadiliko ndani ya jamii.

Afisa Mwakilishi wa Serikali katika NMB,  Domina Feruz, alisema kilimo cha umwagiliaji kitatoa uhakika wa mavuno na kuwapo uhakika wa marejesho ya mkopo na chakula muda wote wa mwaka", alisema Afisa huyo.