Namba 7 ni maarufu sana kwenye kikosi cha Manchester United kwasababu ya kuvaliwa na wachezaji wenye mafanikio makubwa na United. Kuanzia George Best, Cantona, Cristiano Ronaldo.
Pia huwa ni kivutio kikubwa kwa mashabiki wa Manchester united. Griezmann mwenye miaka 25 amekua tangu utotoni akiwa shabiki mkubwa wa Manchester United, pia alikua ana muangalia Beckham kama role model.
Kuna kizuizi kikubwa cha pesa za kulipwa ili kumpata Griezmann lakini Mourihno anaweza kutumia pesa za kumuuza Memphis kama na ziada kumpata Griezmann. Habari nyingine ni kwamba Griezmann amepewa ahadi ya kuvaa jezi hiyo maarufu kwenye historia ya Manchester united. Pia kocha wa Atletico amesema kwamba hawezi kumzuia Griezmann kama anataka kuanza maisha mapya sehemu nyingine.
Antoine amekua chagua la juu la Mourihno na pia ana ukaribu mkubwa na Pogba ambaye yupo kwenye kikosi cha kwanza cha Manchester united. Wakiwa pamoja kwenye kikosi hicho inaonekana kwamba itakua combination nzuri na kuleta matokeo chanya.