SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 29 Novemba 2016

T media news

RAIS DKT.MAGUFULI AMWANDALIA RAIS EDGAR LUNGU DHIFA YA KITAIFA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Rais Mstaafu wa awamu ya Pili AlhajAli Hassan Mwinyi,Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt. Amani Abeid Karume wakielekea kwenye dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa heshima ya Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Lungu katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es salaam usiku huu.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakielekea kwenye dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa heshima ya Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Lungu katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es salaam usiku huu.

Rais Dkt John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Lungu katika ukumbi wa Ikulu kwa dhifa hiyo ya kitaifa aliyomwandalia mgeni wake Ikulu jijini Dar es salaam usiku huu.

Meza kuu ikiwa imesimama kwa Wimbo wa Taifa

Rais Dkt Magufuli akimsindikiza mgeni wake Rais Edgar Lungu wa Zambia kusalimiana na viongozi mbalimbali

Rais Edgar Lungu wa Zambia akisalimiana na Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi. Kulia ni Naibu Spika Dkt Tulia Ackson

Rais Edgar Lungu wa Zambia akisalimiana na Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete

Rais Edgar Lungu wa Zambia akisalimiana na Naibu Spika Dkt Tulia Ackson

Rais Edgar Lungu wa Zambia akisalimiana na Spika Mstaafu Mhe. Pius Msekwa

Rais Edgar Lungu wa Zambia akisalimiana na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman

Rais Edgar Lungu wa Zambia akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt Amani Abeid Karume

Rais Edgar Lungu wa Zambia akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba

Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Bw. Gerson Msigwa akisherehesha hafla hiyo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia

Rais Edgar Lungu wa Zambia akigonganisha glasi na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan

Wimbo wa Taifa 

Viongozi wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Taifa wa Zambia ukipigwa

Viongozi wa vikosi vya ulinzi na usalama pamoja na Mkuu wa Itifaki wa Zambia wakiwa wamesimama kwa wimbo wa Taifa 

Sehemu ya Mawaziri waliohudhuria wakiwa wamesimama

Viongozi wakiwa wamesimama

Makatibu wakuu na sehemu ya ujumbe wa Zambia

Wageni waalikwa na viongozi wa vyama vya siasa

Baadhi ya mabalozi mbalimbali waliohudhuria

Wageni mbalimbali

Mabalozi mbalimbali

Mabalozi na maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje 

Wafanyabiashara na viongozi wa taasisi mbalimbali

Wafanyabiashara na viongozi wa taasisi mbalimbali na maafisa wa Wizara ya Mambo ya nje

Viongozi wa taasisi mbalimbali

Viongozi wa kidini na wageni mbalimbali


Makatibu wakuu na Balozi wa Tanzania nchini Zambia Mhe. Grace Mujuma

Rais Dkt Magufuli akigonganisha glasi na mgeni wake Rais Edgar Lungu wa Zambia

Mrisho Mpoto na Banana Zorro na Mjomba band akitumbuiza


Mrisho Mpoto akighani wimbo maalumu

Rais Edgar Lungu akiagana na viongozi 





Rais Edgar Lungu akiagana na viongozi 

Rais Edgar Lungu akiagana na Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein

Rais Edgar Lungu akiagana na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan

Rais Edgar Lungu akisindikizwa na mweyeji wake Rais Dkt Magufuli

Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt. Amani Abeid Karume wakiondoka baada ya dhifa


Rais Dkt. Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho kikwete na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi wakifurahia jambo mara baada ya dhifa hiyo ya Kitaifa Ikulu jijini Dar es salaam. PICHA NA IKULU