SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumapili, 27 Novemba 2016

T media news

Picha: Makonda atinga 'Uwanja wa fisi' wanapojiuza madada poa


Mkuu wa mkoa wa mkoa wa Dar es Salaam ,Paul Makonda akiangalia barabara ya Tandale inayounganisha eneo la Mwananyamala ambayo imekuwa haihpitiki kwa uraisi kwa kipindi chote kutokana mashimo ya yaliyokithiri  na kupelekea usumbufu mkubwa kwa waendeshaa magari na kwa miguu pia,leo jijini Dar es Salaam. 


Mkuu wa mkoa wa mkoa wa Dar es Salaam ,Paul Makonda akiteta na Mlemavu ambaye amemkuta katika eneo la uwanja wa fisi akinywa pombe za kienyeji na kumsihi aache kunywa pombe hizo, leo jijini Dar es Salaam. 


Mkuu wa mkoa wa mkoa wa Dar es Salaam ,Paul Makonda akiwa ameongozana na Kamanda   wa kanda maalum ,Simon Sirro kugonga nyumba za baadhi ya akina dada  ambao hufanya biashara ya kujiuza katika eneo la uwanja wa fisi, leo jijini Dar es Salaam. 


 Mkuu wa mkoa wa mkoa wa Dar es Salaam ,Paul Makonda akiwa na Kamanda wa kanda maalum ,Simon Sirro wakiangalia bia ambazo zinauzwa uwanja wa fisi zikiwa zimekwisha muda wake,ambazo inaelezwa zimekuwa zikitumika kwa ajili ya matumizi ya Binadamu, leo jijini Dar es Salaam.Picha na Emanuel Masaka-Globu ya Jamii