Rais mteule wa Marekani, Donald Trump, na mgombea wa urais mwaka wa 2012 kwa tiketi ya Republican, Mitt Romney, waliweka kando tofauti zao na kufanya mazungumzo jana, ambayo yanaonyesha dalili kuwa Romney huenda akapewa wadhifa wa waziri wa mambo ya kigeni.
Trump pia alikutana na jenerali mstaafu wa jeshi la Marekani, James Mattis, ambaye anapewa nafasi kubwa ya kuwa waziri wa ulinzi.