SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 2 Julai 2016

T media news

ROBO FAINALI YA TATU EURO 2016: JE, LEO UJERUMANI KUFUTA UTEJA KWA ITALY?


Na Mahmoud Rajab

Robo fainali ya tatu inapigwa inapigwa leo ambapo miamba miwili ya Ulaya Ujerumani na Italy watakuwa na kibarua kigumu kutafuta nafasi ya kutinga nusu fainali, mchezo utakaofanyika kunako dimba la Matmut Atlantique lililopo jijini Bordeaux majira ya saa nne za usiku.

Taarifa muhimu za kila timu

Ujerumani wanaingia katika mchezo wa leo wakiwa na kikosi kamili baada ya wachezaji wao Jerome Boateng, Julian Draxler na Sami Khedira kuwa kupona majeraha yao madogo yaliyokuwa yakiwasumbua.

Italy watakuwa na hati hati ya kutomtumia kiungo wake Daniele De Rossi, ambaye anasumbuliwa na jeraha la paja alililopata katika mchezo dhidi ya Uhispania.

Mbadala wake sahihi Thiago Motta naye hatakuwepo kutokana na kutumikia adhabu ya kukosa mchezo mmoja kufuatia kupata ladi mbili za njano, huku winga Antonio Candreva pia akikosekana.

Endapo De Rossi atashindwa kabisa kucheza mchezo wa leo, basi nafasi yake itabidi izibwe na Stefano Sturaro.

Jambo la hatari zaidi ni kwamba wachezaji takriban 11 wa Italy wana kadi za njano. Wachezaji hao ni Andrea Barzagli, Leonardo Bonucci, Gianluigi Buffon, Giorgio Chiellini, Daniele De Rossi, Mattia De Sciglio, Eder, Lorenzo Insigne, Graziano Pelle, Salvatore Sirigu na Simone Zaza. Na endapo watapa kadi nyingine leo tafsiri yake ni kwamba wataukosa mchezo wa nusu fainali endapo timu yao itafuzu.

Kwa upande wa Ujeruamni Boateng, Khedira, Mats Hummels, Joshua Kimmich na Mesut Ozil wote wana kadi za njano.

Preview

Italy wamekutana na Ujerumani mara nane katika michuano mbalimbali mikubwa duniani na hawajawahi kupoteza hata mchezo mmoja.

Katika michezo minne ya mtoano waliyokutana , wamewafunga Ujerumani kwenye mecho zote nne, huku ya mwisho ikiwa ni ile ya nusu fainali ya Euro mwaka 2012 ambapo Italy walishinda mabao 2-1.

Ni rekodi nzuri sana kwa Italy lakini inayochoma kwa Ujerumani. Lakini safari hii Ujerumani wanaonekana kuja na ‘mentality’ tofauti kabisa kuelekea mchezo wa leo.

“Hatuna hofu na Italy, kwa sababu ni timu tofauti kwa sasa na nadhani kwa sasa hatufikirii chochote juu ya masuala yaliyopita,” kocha wa Ujerumani Joachim Low amesema.

“Tunahitaji kahawa ya baridi na tutahakikisha inakuwa na ladha nzuri sana siku ya Jumamosi (leo),” ameongeza.

Katika mchezo wao wa kirafi uliochezwa mwezi March Ujerumani walionesha ukomavu wa aina yake baada ya kuwatungua Italy mabao 4-1.

Moja ya vita makubwa leo jijini Bordeaux itakuwa katika safu ya ulinzi. Italy wameruhusu goli moja tu mpaka sasa tena goli ambalo lilifungwa wakati mabeki wao visiki maarufu kama BBC Andrea Barzagli, Leonardo Bonucci na Giorgio Chiellini hawakucheza pamoja (kwenye mchezo dhidi ya Republic of Ireland).

Safu ya ulinzi ya Ujerumani nayo si ya kugusa kwani timu timu pekee mpaka sasa kwenye michuano hii ambayo nyavu zake haziguswa na timu yoyote.

Takwimu muhimu katika mechi walizokutana.

Ujerumani hawajawahi kuwafunga Italy katika michezo yote kwenye michuano mbalimbali duniani (sare nne, wamefungwa mara nne).Wamepoteza michezo yao yote minne ya mwisho dhidi Italy kwenye hatua ya mtoano katika michuano mbalimbali – mara tatu katika Kombe la Dunia hatua ya nusu fainali (1970, 2006 na fainali ya mwaka 1982) na mara moja kwenye nusu fainali ya michuano ya Euro mwaka 2012.Mchezo wa mwisho kati ya miamba hii miwili ulipigwa mwanzoni mwaka mwaka huu na Ujerumani kuibuka na ushindi wa mabao 4-1, mchezo uliochezwa jijini Munich. Huo ulikuwa ni ushindi wa kwanza kwa Ujerumani dhidi ya Italy tangu June 1995Magoli 15 kati ya 18 yaliyofungwa kwenye mechi nane zilizopita katika michunao mbalimbali yamefungwa katika kipindi cha pili, yakiwemo saba yaliyofungwa kwenye muda wa ziada (extra time).

Ujerumani

Ujerumani wamefanikiwa kufika angalau hatua ya nusu fainali katika michuano mbalimbali mikubwa mitano iliyopita. Mara ya mwisho kushindwa kufanya hivyo ilikuwa kweye Euro ya mwaka 2004 (walitolewa katika hatua ya makundi).Wameshinda mechi 14 kati ya 17 zilizopita katika michuano yote mikubwa, wakitoka sare mara mbili na kupoteza mara moja (kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Italy kwenye nusu fainali ya Euro mwaka 2012)Ujerumani ndio timu pekee mpaka sasa ambayo haijaruhusu hata goli moja kwenye michuano hii. Mara ya mwisho kufanya hivyo ilikuwa ni kwenye Kombe la Dunia mwaka 1978, ambapo walicheza michezo miine bila ya kuruhusu goli.Mchezaji wa mwisho kumfunga Manuel Neuer katika michuano ya kimataifa alikuwa ni Oscar kwenye fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazil. Hii ni sawa na muda wa dakika 480.Thomas Muller hajafunga goli katika michezo tisa kwenye Euro. Ana magoli 10 kwenye michezo 13 ya Kombe la DuniaMario Gomez amefunga magoli matano katika michuano yote ya Euro aliyocheza. Anafungana na Jurgen Klinsmann na kuwa wafungaji bora wa Ujerumani katika wa muda wote kwenye michuano hii.Gomez ameifungia Ujerumani magoli 21 kwenye michezo yake 27 iliyopita aliyoanza, amefunga goli moja kwenye kwenye kila mchezo alioanza mwaka 2016.Bastian Schweinsteiger anaweza kufikia rekodi ya Miroslav Klose ya kuichezea Ujerumani michezo 37 kwenye Michuano ya Ulaya na Kombe la Dunia kwa pamoja.

Italy

Italy wamepata clean sheets 19 kwenye michezo 37 katika Michuano ya Ulaya, zaidi ya timu yoyote katika historia ya michuano hii. Wamewazidi Ujerumani kwa tofauti ya moja (Ujerumani wamepata clean sheets 18 kwenye michezo 47)Tayari wameshinda michezo mitatu kwenye Euro ya mwaka huu, kiwango cha juu kabisa (ukiondoa changamoto ya mikwaju ya penati) tangu Euro ya mwaka 2000 ambapo walishinda mara nne.Mchezo pekee wa Italy katika mji wa Bordeaux katika michuano mbalimbali ulikuwa ni ule waliocheza dhidi ya Chile katika hatua ya makundi ya Kombe la Dunia na kuisha kwa sare ya 2-2.Andrea Barzagli na Leonardo Bonucci ndio wachezaji pekee kwa Italy walionza michezo yote kwenye michuano hii.Magoli mawili ya Graziano Pelle kwenye michuano hii yamefungwa katika dakika ya 92 na 91.