SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 16 Aprili 2018

T media news

Uda-rt Yafunga Barabara ya Jangwani

Kampuni inayotoa huduma katika mradi wa mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam (Uda-rt), imelazimika kusitisha huduma kwa baadhi ya njia.

Taarifa ya Uda-rt imesema huduma za mabasi hayo kwa baadhi ya njia zimesitishwa kuanzia saa 11:00 alfajiri leo Jumatatu Aprili 16, 2018 kutokana na kufungwa Barabara ya Morogoro eneo la Jangwani.

Barabara hiyo imefungwa kwa sababu ya mafuriko yaliyosababisha maji kupita juu ya daraja la Mto Msimbazi.

“Kwa sasa huduma zinatolewa kwa njia za Mbezi – Kimara; Kimara – Morocco; Kimara - Magomeni Mapipa; Kivukoni – Muhimbili; Gerezani – Kivukoni; na Gerezani – Muhimbili,” inasema taarifa ya Uda-rt iliyotolewa na mkuu wa kitengo cha mawasiliano, Deus Bugaywa.

Kampuni hiyo inasema huduma kamili zitarejea baada ya barabara kufunguliwa.