SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 1 Machi 2018

T media news

Polisi wazuia mkutano wa Mbunge wa CHADEMA

Jeshi la Polisi wilayani Bukoba, limemtaka Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini, Wilfred Lwakatare kuahirisha kufanya mkutano wa hadhara na wananchi wa jimbo lake, kutokana na kile kilichodaiwa kuwa hali ya usalama kutokuwa shwari katika eneo hilo.

Mbunge huyo aliyekuwa amepanga kufanya mkutano jana, Jumatano Februari 28, alipokea barua hiyo kutoka kwa Mkuu wa Polisi Wilaya ya Bukoba, SP. B. S. Sanare iliyokuwa imeandikwa siku moja kabla ya siku ya mkutano, na nakala ikapelekwa kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera pamoja na Mkuu wa wilaya ya Bukoba.