SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 23 Februari 2018

T media news

Yametimia! Safari ya Akwilina Yafika Mwisho Azikwa Kijijini kwa Wazazi Wake

Mwili wa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini umezikwa nyumbani kwa wazazi wake kijiji cha Olele wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro.

Akwilina aliyeuawa Februari 16, 2018 amezikwa leo Februari 23, 2018 saa 8:45 mchana na mamia ya waombolezaji baada ya kumalizika kwa ibada ya mazishi iliyofanyika kanisa la Mtakatifu Theresia Parokia ya Olele.

Baada ya uwekaji maua katika kaburi, watu mbalimbali wakiwemo wanafamilia watatoa salamu za rambirambi.