Serikali ya Burundi imepiga marufuku upigaji wa ngoma katika mikutano isiokuwa rasmi ikiwemo sherehe za kitamaduni na harusi katika jaribio la kuhifadhi mila hiyo ya zamani ambayo inajuliakana kimataifa.
Makundi yote yanayotaka kufanya tamasha za kitamaduni sasa yatalalizimika kujisajili na wizara ya Utamaduni na hayataruhusiwa kupiga ngoma kando na mikutano rasmi ya serikali bila ruhusa , agizo ambalo limetiwa saini na rais Pierre Nkurunziza.
Agizo hilo pia linapiga marufuku wanawake kupiga ngoma.
Hairuhusiwi kwa wanawake kupiga ngoma.
Hatahivyo wanaweza kushiriki katika kucheza densi za kitamaduni wakiandamana na ngoma hizo, kulingana na chombo cha habari cha AFP kilichonukuu agizo hilo.
Hilo ni jaribio la kusitisha na hatua mpya ya wanawake wa Burundi kupiga ngoma.
Kitamaduni wanawake hawakuruhusiwa kupiga ngoma nchini Burundi.
Ngoma inaonekana kama yenye umbo la mwanamke.
Agizo hilo pia linasema kuwa kundi lolote litakalotaka kupiga ngoma katika nchi za ugenini litalazimika kupata ruhusa kutoka kwa wizara.
Densi ya Burundi inatambulika na shirika la Umoja wa mataifa kuhusu Utamaduni Unesco kama urithi wa utamaduni isioonekana.
Mila hiyo inasemekana kuamsha roho za mababu na kufukuza pepo wabaya.