Mtandao wa kutuma mafaili mbalimbali kama Picha, Video na Sauti wa WhatsApp umekwama kufanya kazi kwa masaa kadhaa kwenye baadhi ya nchi duniani ikiwemo Tanzania.
Ripoti zinasema tatizo hilo limeanzia nchini Uingereza kisha kuendelea katika nchi za Marekani, Italia, Ujerumani India na sasa nchi za Afrika Mashariki nazo zimepitia changamoto ya kukosa huduma ya mtandao huo.
Tatizo hilo limeelezwa kuanza majira ya saa mbili asubuhi ambapo maelfu ya watumiaji wa WhatsApp wameeleza kukosa huduma. Wengi wao wamelalamika kukwama kwenye baadhi ya majukumu yao kutokana na kutegemea mtandao huo kwaajili ya kuhamisha na kupokea mafaili yao.
Hadi sasa bado wamiliki wa mtandao huo ambao ni kampuni ya Facebook chini ya Mkurugenzi Mark Zuckerberg hawajatoa tamko juu ya tatizo hilo.
Update
WhatsApp imerejea kwenye hali ya kawaida hapa Tanzania, wakati huo nchi zingine kama Uingereza bado zinalalamika kukosa huduma hiyo ambapo watumiaji wanasema inafunguka na kuonesha kuwa kuna ujumbe umeingia lakini hauwezi kuufungua ili kuusoma au kuona kama ni Picha au Video.