SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 11 Septemba 2017

T media news

Ibrahim Mo atamfukuzisha  kazi Omog pale Simba

Na  Baraka Mbolembole

KATIKA uchambuzi wa kwenye makaratasi, Simba SC walionekana kuwa na kikosi cha ‘kutisha’ na tena walikuwa na wachezaji wengi ‘maarufu’ kuliko Azam FC, lakini hayo hayakuweza kumsaidia kitu kocha wa timu hiyo Mcameroon, Joseph Omog kufikia ‘matarajio.’ Naamini hilo baada ya mchezo kumalizika kwa suluhu-tasa Jumamosi iliyopita.

‘Ubutu’ wa washambuliaji wa omog haukuanza leo

Kuna mengi yamebadilika katika safu ya mashambulizi ya Simba tangu kuondoka kwa Mrundi, Amis Tambwe mwezi Disemba, 2014. Elius Maguli na Emmanuel Okwi walisajiliwa katikati ya mwaka 2014 mara baada ya uongozi wa Evance Aveva na Geofrey Nyange Kaburu walipoingia madarakani.

Maguli alikuwa ametoka kufanya vizuri katika kikosi cha Ruvu Shooting, na Okwi alisajiliwa akitokea Yanga SC ambako alicheza kwa miezi sita msimu wa 2013/14. Usajili huu ‘niliuita usio wa kimpira’ kwa sababu tayari Simba ilikuwa na vijana kama Edward Christopher, Ibrahim Ajib na Mbaraka Yusuph huku Tambwe akitoka kufunga magoli 19 na kushinda tuzo ya ufungaji bora msimu wa 2013/14.

Maguli alifeli Simba kwa maana alifunga magoli manne tu, huku Okwi akifunga 12 kwa msimu mzima na Tambwe ambaye aliondoka wakati wa usajili wa dirisha dogo na kujiunga Yanga akimaliza msimu akiwa na magoli 15, huku mawili tu akifunga akiwa Simba.

‘Angaika angaika’ ya usajili ikifanikiwa kupata suluhisho katika safu ya mashambulizi ya Simba baada ya kumsaini  Mganda, Hamis Kizza, lakini jambo la ajabu Kizza alikja kuachwa mwishoni mwa msimu licha ya kufunga magoli 23 katika ligi  (magoli ( 19)  na michuano ya FA (magoli manne)

Kiiza aliachwa kwa sababu za ‘kufikirika’ kuwa ‘mtu wa Yanga’ na mashabiki wakasapoti hilo bila kutazama idadi ya magoli yake aliyofunga. Ujio wa Mrundi, Laudit Mavugo katikati ya mwaka 2015 ulimuondoa Kizza,huku ujio wa Kizza Julai, 2015 ukimuondoa Okwi, na ujio wa Okwi ukimuondoa Tambwe.

Naweza kusema bila shaka yoyote kuwa katika kipindi cha misimu hii minne Simba ndiyo timu iliyotumia kiasi kikubwa sana cha pesa kusajili washambuliaji lakini imekuwa ‘butu’ kuliko safu za mashambulizi za Yanga na Azam FC kwa misimu hii ya karibuni.

Na yote haya wakati mwingine yanachangiwa na ‘usajili wa kina Mr.Kazinyingi’ ndiyo maana licha ya ujio wa majina makubwa na wafungaji waliofanya vizuri katika timu nyingine ‘Msimbazi hapo’ pamekuwa ‘chungu cha moto.’

Mavugo nilimuhurumia msimu uliopita alipoangaika kutimiza ahadi yake ya kufunga magoli 30 katika msimu mmoja wa VPL. Maskini aliishia kufunga magoli  nane tu na sasa amekuwa ‘mkosa magoli hatari’ wa Simba na kuwachosha hadi mashabiki wa timu yake ambao walimlinda sana na kusema ‘apewe muda zaidi.’

Upande sutaki kuona  Mavugo akipewa muda bali tujiulize kwa nini washambuliaji waliofanikiwa zaidi Simba ndani ya  misimu minne iliyopita hawakupewa muda, na tuwape muda ‘wachovu’ waliosajiliwa kwa matakwa Fulani Fulani tu ya watu?

Sioni kipya kutoka kwa Mrundi huyu, na itakuwa mafanikio sana kwake kama atafunga magoli nane msimu huu kama tu timu hiyo itaendelea kunolewa na Omog ambaye naweza kusema alikubali usajili ambao ‘hawezi kuufanya utoe matunda’ kwa timu yake.

Kukubali rundo la washambuliaji wenye majina makubwa nchini si kigezo cha timu nyingine kupoteza mechi vs Simba. Labda kama Omog alikubali ujio wa Okwi, Mghana, Gyan, John Bocco, Mavugo, Juma Liuzio kwa kuamini majina yake yatampa ushindi katika mechi.

Lakini kama alihitaji ushindi baada ya washambualiaji wake kufunga  hakupaswa kuwa na washambuliaji wote hao wakati alishuhudia viungo wake Shiza Kichuya, Mohamed Ibrahim na Muzamiru Yassin wakifunga zaidi ya magoli 25 msimu uliopita. Katika hili hawezi kukwepa lawama, kamani usajili wake watu wanataka kuona matunda haraka kwa maana walishamsubiri msimu uliopita. Omog amejipa mzigo mkubwa sana na  ataangaika sana kupata pacha ya mashambulizi hadi atakapofukuzwa.

Angeamua tu kuchagua washambuliaji watatu. Sasa tangu wakati wa maandalizi ya msimu Simba hii ‘mnayosema ya kutisha’ imekuwa na tatizo kubwa la ufungaji, lakini linaweza kutatulika ikiwa wachezaji wa kikosi hicho watapata kocha mpya haraka kwa sababu mbinu za Omog haziwezi kuwafanya wafungaji wafunge, labda siku kikosi kikipangwa na msaidizi wake Mganda, Jackson Mayanja ambaye yeye hupendelea soka la kushambulia na kuzuia kwa kutegemea umiliki wa mpira.

Njia mbadala ya simba kupata magoli

Vikosi vya Omog pale Azam FC havikuwa na makali katika ufungaji, msimu wake wa kwanza Simba timu ilikuwa butu kiufungaji. Tatizo hapa ni yeye na mbinu zake. Kwa aina ya wachezaji alionao Omog anapaswa kushikilia zaidi mfumo wa 4-3-2, na kuutumia mfumo wa 4-4-2 wakati anapohotaji kuwatumia washambuliaji wawili.

Katika 4-3-3 hapa, haitaji kuwa na mfungaji asilia lakini atahitaji wachezaji kama Okwi, Kichuya, Mohamed Ibrahim ambao wana ‘unyumbulifu’ mkubwa  ambao unaweza kupasua ngome ngumu kama ile waliyokutana vs Azam FC Jumamosi iliyopita ama Yanga katika mchezo wa Ngao ya Jamii. Wote hawa wana shabaha, wanapenda kufunga magoli na kupiga pasi zisizotarajiwa.

Mara ya mwisho niliiona Simba kali wakati Okwi,Haruna Moshi ‘Boban’ wakicheza katika 4-3-3 wakimzunguka Mzambia Felix Sunzu. Nyuma yao kulikuwa na viungo wachezesha timu wenye ubunifu mkubwa marehemu, Patrick Mafisango, Mwinyi Kazimito na SalumMachaku.

Najua, Omog anahofia kumuweka benchi Okwi,na amekuwa akimuamini sana Kichuya ndiyomaana Mo Ibra amekuwa akikosa nafasi ya kuanza, lakini angetambua umuhimu wa Mo Ibra katu hasingeweza kumuweka benchi mchezaji huyo ambaye alimnyanyua sana msimu uliopita.

Jonas Mkude ameshapoteza nafasi yake kwa Mghana, James Kotei na mambo yanakwenda, kumuacha nje ya kikosi cha kuanza mchezo Muzamiru ni sawa na kuinyima ushindi timu yako, na si rahisi kuona Mnyarwanda, Haruna Niyonzima akikosa nafasi ya kuanza kikosi anapokuwa fiti kimwili na kiakili.

Kotei, Haruna, Muzamiru hapa tayari Omog amefanikiwa katika 4-3-3, lakini bado ameshindwa jinsi ya kupanga watatu watatu wa mbele katika mashambulizi, na hofu ya mapokeo ya mashabiki ndiyo inampa shaka ya kupanga vizuri safu ya mashambulizi kwa kudhani atalaumiwa sana ikiwa wachezaji Fulani watashindwa kuanzishwa.

Ningekuwa katika nafasi yake ningewapanga, Okwi, Kichuya na Mo Ibra na kama ningetumia mfumo wa 4-4-2 ningewapanga Kotei, Haruna, Muzamiru na Mo Ibra huku Bocco na Okwi, ama Bocco na Liuzio, ama Okwina Liuzio, nap engine Mavugo na Okwi.

Mo Ibrahim atamfukuzisha kazi haraka Omog

Endapo Simba itashindwa kufunga walau magoli manne katika michezo yake mitano ijayo si ajabu Omog akawa nje ya kikosi baada ya mchezo vs Yanga . kabla ya kuwavaa mahasimu wao hao Simba itacheza na Mwadu FC katika uwanja wa Uhuru, itaenda nje ya Dar es Salaam kwa mara ya kwanza kucheza na Mbao FC Septemba 21, watapia Sinyanga kucheza na Stand United kasha kurejea Dar kucheza na Mtibwa Sugar FC, Mjombe FC na Yanga.

Ni ratiba nyepesi kwa timu inayopangwa vizuri kama Simba lakini kwa aina ya mchezo wa kikosi hicho chini ya Omog ratiba hiyo itakuwa ngumu na huenda ‘ikamsomba’mtu kama mafuriko. Omog akubali kuwa Mo Ibra hapaswi kuwekwa benchi anapokuwa timamu kimwili na kiakili. Akiendelea kuwakumbatia mastaa wasio na msaada kifungaji mashabiki hao hao anao wahofu wataanzisha kelele za kushindwa kwake.

Mo Ibra anacheza upande wa kushoto vizuri sana, anajua kushambulia akitokea kulia na mpigaji wa pasi bora za mwisho akitokea katikati ya uwanja. Sawa Ndemla anahitaji kusuburi, lakini ni hatari kufanya hivyo kwa wakati mmoja ukimuhisha na Mo Ibra.

Huyu anaweza kmtete kocha asiye na mbinu bora za ufungaji pale Simba, lakini ni huyu huyu Mo Ibra ambaye atamuondoa haraka Omog pale Simba. Mpe nafasi kijana huyu atengeneze utulivu katika ufungaji.