SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 8 Septemba 2017

T media news

Bundesliga nao wafuata nyayo za TFF kuhusu waamuzi wa kike

Wakati Tanzania tukionesha mfano kwa kuwa na muamuzi  Jonesia Rukyaa ambaye ameshawahi kuchezesha mapambano ya ligi kuu ikiwemo mpambano wa watani wa jadi kati ya Simba na Yanga, wenzetu Ulaya walikuwa bado.

Lakini ligi kuu nchini Ujerumani Bundeslgia imeiga mfano wa Tanzania na sasa wameamua kumuweka muamuzi wa kike kwa mara ya kwanza katika ligi hiyo na Jumamosi ya wiki hii atakuwepo uwanjani.

Bibie Bibiana Steinhaus atakuwa muamuzi wa kwanza wa kike kuchezesha pambano la ligi kuu ya Ujerumani ambapo atachezesha mchezo kati ya Hertha Berlin ambao watakuwa wakikipiga dhidi ya Werder Bremen.

Bibiana ambaye tangu mwaka 1999 amekuwa muamuzi lakini alikuwa akishiriki tu michezo inayohusu wanawake na sasa kwa mara ya kwanza anakwenda kusimama uwanjani kuamua mechi inayohusu wanaume tena ya ligi kuu.

Bibiana tayari ana historia ndefu katika soka la wanawake kwani amekuwa muamuzi katika michezo ya kombe la dunia la wanawake lakini pia mwezi June alikuwa muamuzi wakati wa mechi ya fainali ya wanawake katika Champions League.

Ujio wa Bibiana katika ligi kuu ya Bundesliga umepokelewa kwa mitazamo tofauti kwani kocha wa Hoffeinman amefurahia na kusema mwanamama huyo anastahili huku baadhi ya mashabiki wakipinga uwepo wa mwanamke katika mchezo wa wanaume.