SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 22 Juni 2017

T media news

Shomari Kapombe atoa onyo kwa timu za ligi kuu

Na  Zainabu Rajabu.

BEKI mpya wa Simba, Shomari Kapombe anaamini Simba itafanya vizuri msimu ujao na kuwa timu tishio katika ligi kuu na hata kuweza kuchukua ubingwa wa ligi kuu ya Tanzania.

Kapombe amesaini kuichezea Simba kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Azam yenye maskani yake Chamazi Complex ambapo ni ka amerejea nyumbani kwani alikuwa Simba hapo kabla.

Shaffidauda.co.tz.ilizungumza na Kapombe amesema Simba imeanza kuonyesha kweli inataka kurudisha kikosi chake, hivyo naamini tutafanya  vizuri.

“Ukiangalia usajili unaofanyika sasa na kikosi kilichopo, hakuna ubishi kwamba Simba itakuwa na kikosi kizuri ambacho kitakuwa tishio hivyo wapinzani wetu wajipange tumekuja kufanya kazi kurudisha ile Simba ya Zamani ambao ilikuwa haina mpinzani katika ligi hii” amesema Shomari.

Mchezaji huyo ambae amerejea  (Simba) amesema anaamini kwa aina ya kikosi walichonacho kwa sasa wapinzani wao watakuwa na wakati mgumu sana wakikutana nao.