SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 21 Juni 2017

T media news

Serikali kuanza kupima utendaji watumishi wake kama zifanyazo kampuni binafsi

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Angellah Kairuki amesema kuwa kuanzia Julai 1 mwaka huu, Serikali itaanza kuwafanyia tathmini ya kazi (performance audit) watumishi wake wote ili kubaini wanaofanya kazi sawasawa na wake wanaofanya kwa mazoea.

Amesema kuwa, mifumo yote ya kusimamia utaratibu huo imeshashughulikiwa na imekamilika, hivyo, watumishi wote wa umma watambue kuwa kuanzia tarehe moja watakuwa wakifanyiwa tathmini ya utendaji wa kazi zao.

Utaratibu huu utakuwa ni mpya kabisa kwa wafanyakazi wa Serikali nap engine unaweza kuwa mchungu sana kwao, lakini kwa wale walio kwenye ajira za sekta binafsi, huu si utaratibu mpya. Katika tathmini ya mfanyakazi mmoja mmoja, mwanzo wa mwaka viongozi wa Idara hukaa na wafanyakazi walio chini yao kujadili viwango na alama anazotakiwa kuzifikisha kiutendaji ili aendelee kuwa mwajiriwa wa kampuni husika – na mara nyingi inatishia kupoteza ajira yako kama utapata alama chini ya wastani uliowekwa au unaotegemewa kutoka kwako.

Hii inasababisha makampuni binafsi kufanya vizuri na wafanyakazi wake kufanya kazi kuzingatia taaluma zaidi katika utoaji wa huduma. Pengine kwakuwa hali halikuwa likifanyika serikalini, wengi watakwenda na maji kwa mazoea yao ya “njoo kesho, faili halionekani.”

Kwa upande mwingine, akijibu swali kuhusu maneno yaliyoenea mitaani kwamba Serikali imesitisha ajira, Waziri Kairuki amesema kuwa serikali inaendelea kuajiri kwenye maeneo mbalimbali na kwamba itakuwa ikifanya hivyo awamu kwa awamu.

“Niwatoe hofu wahitimu kwamba wawe watulivu tu, ajira zipo na zitaendelea kutolewa kwa kada mbalimbali. Tumeshatangaza ajira 52,000 kwenye bajeti hii na watumishi 9,000 tayari wameajiriwa,” amesema.