Rais Dkt John Pombe leo ametengua uteuzi wa aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kwa kile alichosema kuwa ni kushindwa kusimamia wizara hiyo na hivyo kupelekea serikali kupata hasara kufuatia makinika ya madini kusafirishwa kwenda nje ya nchi.
Rais ametoa uamuzi huo baada ya kupokea ripoti kutoka kwa kamati aliyoiunda kuchunguza kiasi cha madini kilichomo kwenye mchanga wa madini unaosafirishwa nje ya nchi.
Baada ya Rais Magufuli kutengua uteuzi huo, watu mbalimbali wakiwamo viongozi na wabunge wamekuwa na maoni mbalimbali juu ya kutengua uteuzi huo na pia kuhusu ripoti iliyowasilishwa kwake leo. Hapa chini ni baadhi ya maoni kutoka kwenye mitandao ya kijamii.