Serikali ya Marekani, wiki hii imewarudisha makwao raia watano wa Kenya na raia 67 wa Somalia kwa kukosa vigezo vya uhamiaji.
Shirika la habari la BBC limemnukuu afisa mmoja wa Serikali ya Kenya akieleza kuwa watu hao wemewasili leo katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta.
Hatua hiyo ya kutimuliwa kwa raia wa nchi hizo mbili ni matokeo ya oparesheni maalum ya Marekani iliyoasisiwa na Rais Donald Trump kuwashughulikia raia wote wa kigeni wanaoishi nchini humo kinyume cha sheria na taratibu za uhamiaji.
Hili ni kundi la pili la raia wa nchi hizo kutimuliwa kutoka Marekani. Januari 2017, raia wawili wa Kenya na raia 90 wa Somalia walitimuliwa kutoka Marekani kwa sababu za uhamiaji.
Rais wa Marekani, Trump alianza na kupigilia msumari kwa sekta ya uhamiaji nchini humo huku akitangaza marufuku ya siku 90 kwa raia wa Iran, Iraq, Libya, Somalia, Sudan, Syria na Yemen kuingia nchini humo.