Msanii anayefanya poa sana kwenye muziki wa singeli 'Man Fongo' amepinga vikali kauli zinazotolewa ya kwamba muziki wa kisingeli unaweza ukapotea muda wowote na kudai wenye dhamana na muziki huo wameshaubariki hivyo ni vigumu kupotea.
Man Fongo amefunguka hayo kwenye 5 Selekt ya EATV na kusema kuwa kamwe muziki wa singeli hauwezi kupotea kwani asili yake ni uswahilini na kwa kuwa waswahili wameshaushikilia itakuwa ni vigumu hivyo wapenzi wa singeli waendelee kuonyesha sapoti.
"Sisi wasanii wa singeli tunapambana kwa sasa kwa kutengeneza video kali na muziki mzuri. Kwa vile pia tupo wachache lazima tuinuie vipaji vya mitaani lazima na sisi tutadumu kama bongo fleva. Singeli haiwezi kupotea kwa sababu chimbuko lake uswahilini, kabla ya kuvuma tayari ulishakuwa na wapenzi wengi mtaani, na kwa vile wao kwa sasa ndio wameubariki na kushikilia juu basi amini hauwezi kupotea"- Manfongo alifunguka.
Pamoja na hayo manfongo amesisitiza upendo kwa wasanii wenzake na kuwasihii umoja wao ndio utakaowafanya waonekane kwenye ramani ya muziki hapa nchini.