SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 25 Mei 2017

T media news

Mpambe wa Diamond Platnumz afukuzwa WCB


Aliyekuwa mwanamitindo wa Diamond Platnumz na timu ya WCB, Q Boy Msafi amethibitishwa kutokuwapo ndani ya lebo hiyo baada ya kufutwa kazi kutokana na kosa alilofanya.

Q Boy amesema kuwa alifanya kosa ambalo linahusu gari la Zari (mpenzi wa Diamond Platnumz) na licha ya kuwa kosa lile ni la kibinadamu kwamba yeyote angeweza kulifanya, lakini uongozi wa WCB uliamua kumfuta kazi.

Q Boy alitoa kauli hiyo akifanya mahojiano na kituo kimoja jijini Dar es Salaam ambapo alisema kwa sasa anajikita zaidi katika kazi zake za muziki, na pia anawashukuru mashabiki kwa kumpokea vizuri.


Q Boy Msafi.

Akizungumzia uhusiano wake na WCB, Q Boy amesema wale ni kama ndugu zake, hana ugomvi nao na kuwa wamekuwa msaada kwake hata baada ya yeye kutoka.

Amefafanua kwamba, hata alipotoa wimbo wake, timu ya WCB haikusita kumsaidia katika mambo mbalimbali. Lakini pia aliweka bayana kwamba yeye ndio anaanza muziki, na anategemea msaada wao sana ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha wasanii wa WCB kama Rayvanny, Rich Mavoko, Harmonize hivyo hawezi kuwa na ugomvi nao.

Aidha, Q Boy amesema kuwa uongozi wa WCB umemtaka aendelee na kazi zake za muziki, na endapo patakuwa na uhitaji wowote wa masuala ya mitindo basi watamtafuta.