SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 10 Mei 2017

T media news

MILNER: Liverpool Tukikosa ‘Top 4’ Nitaugua..!!!


Nahodha msaidizi wa Liverpool James Milner amesema ataugua endapo watakosa nafasi ya kumaliza wane katika Ligi Kuu ya England.

Mliner ameongeza kuwa kuikosa ligi ya mabingwa msimu ujao ni jambo ambalo hapendi kulisikia masikio mwake. Milner alikosa mkwaju wa penalti katika mchezo ambao kikosi cha Jurgen Klopp kililazimishwa sare tasa na Southampton.

Milner ameongeza kusema Liverpool ni timu ambayo inapaswa kucheza ligi ya mabingwa na sio kwingineko. Hata hivyo amesisitiza kuwa anapaswa kuwajibika kwa kukosa mkwaju wa penalti kwenye mchezo huo dhidi ya Southampton.