SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 24 Mei 2017

T media news

Maajabu.. Waungua kwa Kuchomwa Moto Bila Nyumba Kuungua.. Inasadikika Walifumaniwa..!!!


Watu 2 wa jinsia ya kike na Kiume ambao bado majina yao hayajatambulika wamekutwa wamepoteza maisha katika Kitongoji cha Elkiurei Kata ya Kiranyi wilayani Arumeru kwa kile kinachosemekana kuwa ni ajali ya moto.

Akithibitisha tukio hilo mwenyekiti wa kitongoji hicho Bwana Enesphori Chami amesema kuwa tukio hilo ni la kushangaza kwasababu wamekuta marehemu hao katika mazingira ya ya kujiuliza maswali mengi kwa kuwa mwanaume alikuwa amefungwa kamba mikononi jambo lonaloleta utata kuelewa nini kilikuwa kinaendelea.

Bwana Chamia amesema marehemu hao walikuwa mwanaume na mwanamke wanaokadiriwa kuwa na umri wa miaka kata ya 30 na 35 lakini kinachoshangaza wameungua wao pamoja na Godoro jambo ambalo linatia wasiwasi majirani waliokuwa eneo hilo.

Naye shuhuda aliyejionea tukio hilo amesema kuwa walilazimika kuvunja mlango kwa kuwa ulikuwa umefungwa kwa ndani lakini dirisha lilikuwa limefunguliwa jambo ambalo hawajaelewa kwasababu marehemu hao mwanaume alikuwa amefungwa kamba.

Shuhuda huyo amesema kuwa Mwanamke huyo anajulikana kwasababu wako naye siku zote lakini mwanaume anaonekana kuwa ni mgeni kwasababu hawajawahi kumuona na mwanamke alikuwa anaishi peke yake.

Naye Diwani wa kata ya Kiranyi Bwan John Seneu amesema kuwa tukio hilo ni la kushangaza kwasababu kama ni nyumba kuungua ingeteketea yote lakini kilichoungua ni godoro peke yake kitu kinachoendelea kuwafanya wananchi kuwa na maswali mengi.

Hata hivyo ametoa wito kwa wananchi kuendelea kuwa makini Na matukio kama haya na kutambua wageni wanaowatembeleakatika maeneo yao 

Pamoja na hayo jeshi la polisi linaendelea na upelelezi ili kubaini chanzi cha tukio hilo la kusikitisha.