SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 10 Mei 2017

T media news

IPATE Hii Orodha ya Vinywaji & Vyakula Vitakavyoongeza Kinga Zako za Mwili..!!!


Mara nyingi tumekuwa tukipokea maswali kuhusu maana ya kinga ya mwili wengi wakihitaji kujua kinga hizo ni kitu gani na zinaweza kuimarishwa vipi.

Kimsingi kinga za mwili huweza kupanda au kushuka kutokana na chakula unachokula au vinywaji unavyokunywa, lakini pia hata mazingira mazima ya maisha kwa ujumla

Mwili ulibuniwa na Mungu uweze kujitibu wenyewe bila kuhitaji dawa yoyote isipokuwa mwili unaweza kupambana na matatizo kutokana na vyakula unavyokula na kunywa. Shida ni kuwa watu wengi hatujuwi tule nini kwa ajili ya nini, mara nyingi tunakula ili tushibe.

Fanya chakula kiwe ndiyo dawa zako na si dawa kuwa chakula kwako. Kinga yako inapokuwa na nguvu ya kutosha huwezi kuugua ugonjwa wowote kirahisirahisi.

Vifuatavyo ni vyakula 14 vinavyoweza kukusaidia kuongeza kinga za mwili.

Matunda

Katika mlo wako wowote jitahidi usiache kujumuisha angalau tunda la aina moja. Kwa mujibu wa wataalamu wa afya, mtu asiyekula matunda ana hatari kubwa zaidi ya kupata magonjwa zaidi ya mlaji wa matunda.

Asali

Asali halisi husaidia kuimarisha pia kinga za mwili, lamba kijiko kimoja cha chakula kila siku kutwa mara tatu kwa mwezi mmoja itasaidia kuimarishakinga zako za mwili.

Juisi ya ubuyu

Pata kikombe kimoja cha juisi ya ubuyu kila siku kwani juisi hiyo inawingi wa vitami C nyingi ambazo husaidia pia kuimarisha kinga za mwili.

NaziMatumizi ya nazi huweza kusaidia kuimarisha kinga za mwili kutokana na kuwa na mafuta yaitwayo ‘medium chain fatty acids’ ambayo husaidia kuimarisha kinga ya mwili na hivyo kuupa mwili uwezo wa kuyashinda maradhi mbalimbali.

Tangawizi

Ni moja ya kiungo ambacho kinaingia kwenye orodha hii ya kuimarisha kinga za mwili pia.

Mtaalam Mandai anaeleza kuwa ukiona umeshindwa kabisa unaweza kuwasiliana naye ili akupatie moja ya kirutubisho murua ambacho huweza kusaidia kuongeza kinga za mwili (kipo hapo chini kwenye picha)