SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 26 Mei 2017

T media news

Harmorapa Azungumzia Sababu ya Kuvaa Gauni la Bosi Wake..!!!!


Jina la Harmorapa limeingia tena kwenye mzunguko wa kinachojadiliwa mtandaoni, lakini wakati huu akituhumiwa kuvaa gauni la bosi wake na kujiachia nalo kwenye kipande cha video akiimba ‘Vulindela’ ya Brenda Fassie.

Rapa huyo amefunguka kuhusu uamuzi wake wa kuvaa gauni na kujirekodi akidai kuwa alijisikia tu kufanya hivyo akifuata nyayo za alichokifanya Ali Kiba kwenye kipindi cha ‘Lip sync battle’ cha MTV.

“Mimi nilifanya kama cover kwa sababu nakubali anachokifanya Ali Kiba na pia namkubali sana. Kuna wengi huwa wanafanya cover lakini kwa sababu hii amefanya Harmorapa basi ndio maana imekuwa hivyo,” alisema.

Hata hivyo, mkali huyo wa ‘Nundu’ alikanusha kutumia gauni la bosi wake katika kile alichokifanya, huku akisisitiza kuwa hayuko karibu naye kwa muda mrefu.

Harmorapa ‘the entertainer’ kama navyoitwa na P-Funk Majani ni miongoni mwa marapa wachache sana wenye vijimambo na aliyefanikiwa kuvuta usikivu wa watu wengi huku akichukua muda wao kumjadili.

Ni mijadala hii ndiyo inayompa nafasi rapa huyo kuendelea kufanya vizuri akipata kazi za kutumbuiza kwenye majukwaa katika sehemu mbalimbali nchini, akipiga nyimbo zake mbili ‘Kiboko ya Mabishoo na Nundu’.