SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 12 Mei 2017

T media news

DR Mashinji Kwa Haya Hufai Kuwa Katibu Mkuu CHADEMA

Samahani kama nitakukosea ila ukweli lazima ni useme. Naomba nieleweke mimi siyo mfuasi wa chama chochote bali ni.mfuasi wa kiongizi bora toka chama chochote.

Nimejikita katika vipengele vifuatavyo:-

1. HOJA
Mimi binafsi nimefuatilia uongozi wako toka mwanzo, kwa sasa nimeridhika kabisa bila shaka kuwa hufai kuwa Katibu mkuu wa chama kinacho itafuta dola. CHAMA kimekosa ubunifu. CHADEMA imekosa hoja za msingi kupambana na serikali. Serikali imekuwa ikionekana njema licha ya maovu kukithiri. Hoja za msingi zimebaki kwa T. Lissu pekee huku akiatarisha maisha yake. Wekezeni katika kutafuta Scandal mbalimbali za CCM au serikali ili muwe Popular. Chama ni uwekezaji. Wafundisheni wabunge wenu jinsi ya kujenga hoja. Pia wapatieni HINTS zenye ushahidi tosha mf CAG REPORTS.

2. NIDHAMU NDANI YA CHAMA

Nidhahiri ndani ya chama kuna kutokuelewana au mpasuko mkubwa sana. Chama ni mali wa watu na si taasisi. Mf. Saed Kubenea kupitia Magazeti yake ya MAWIO/MWANAHALISI aliwahi kuandika kuwa Ben Saanane ameonekana mitaani na atafuta kiki tu wala hajatekwa, hii ni ishara mbaya sana ndani ya chama. Mimi binafsi natambua na nakiri mchango mkubwa sana wa SAED KUBENEA kuichamba CCM na kuineza CHADEMA toka miaka ya 2000 hadi kufikia kumwagiwa Tindikali. kusameana ni jambo la mhimu sana.

Kuna vijana kama MALISA GJ na timu yake wamekuwa wakiposti hoja au vitu vya hovyo hovyo Fb na mitandao mbalimbali dhidi ya Wabunge (hasa Saed Kubenea) au wanachama wenzao. Hujawahi kuwa kemea ndio maana wanaendelea. Hii ni dhahiri umeshindwa kudhibiti nidhamu ndani ya chama. Jenga chama kama taasisi na si SACCOS ya watu. Vijana wadogo kama Malisa na wengine wote wadhibitiwe mapema.

3. UCHAGUZI EALA

Uchaguzi huu ni dhahiri wewe kweli ni Daktari wa binadamu siyo wa siasa. CCM ni mabingwa wa hujuma, wanafiki, nk lakini hilo ulijidai hulijui!! (Hawa wanacheka na wewe dk1; dk inayo fuata wana kucheka-mpuuzi yule.

Binafsi kwa mtizamo wangu ungepeleka majina 3 tu.
1. EZEKIAH WENJE
2. LAWRENCE KEGO MASHA
3. JOSEPHINE L.

Namuondoa Pamela coz hafai na hana sifa kuwa Mbunge EALA. Alipaswa asubiri hadi 2020 awanie viti maalum Tz au awanie Jimboni. Uwezo wake bado ni mdogo na English hajui ikumbukwe lugha katika EALA ni English. Hapa nahisi kuna mahusiano yapo nyuma ya huyu binti. Pia kuna kampeni kubwa sana ilipigwa ndani ya chama kumpitisha. Kwa style hii vijana wazuri watazidi kujiondoa na kurudi CCM. Yaani mnawakatisha tamaa.

Nitumie nafasi hii kuishauri CHADEMA kuwa Makini sana na Dr. Mashinji. Huyu na JPM ni kanda moja, kamwe hawezi kumtupa. Itakula kwenu endeleeni kusinzia usingizi wa Nyangumi mtashituka 2020 hii hapa mnapigwa KO.

Mungu ibariki Tz.

Written by Enzymes/JF