SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 24 Mei 2017

T media news

Baada ya Star Tv Kurusha Mahojiano na Makonda..Gwajima Aibuka na Madudu Mapya Kuhusu Makonda na Mmiliki wa Star Tv..!!!


Baada kuwa kimya kwa muda na kuacha kuzungumzia suala la Bashite, Mchungaji wa Kanisa la Ufufu na Uzima, Josephat Gwajima asema, “dude limewashwa”   na kwamba  anatarajia kuibua suala hilo tena.

Mchungaji huyo ambaye mapema Machi mwaka huu akiwa kwenye mahubiri kanisani kwake, alidai kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda anatumia cheti cha kidato cha nne chenye jina la Daudi Albert Bushite.

Gwajima ambaye alitajwa kwenye orodha ya Makonda kuhusu sakata la dawa za kulevya, amesema atafufua aliyoyasema Makonda ‘Bashite’ wakati wa mahojiano kati yake na kituo cha televisheni cha Star tv yaliyofanywa Jumatatu.

Gwajima amesema, “ Dude limewashwa, nifafanua aliyoyasema Bashite,  nitaelezea uraia na mmiliki wa kituo cha tv alichokitumia Jumatatu, nitaeleza ukwepaji kodi wake na vyeti vya watangazaji wake na mishahara yao.