Msanii kutoka kundi la Weusi, Nikki wa Pili, amendika ujumbe unaoandamana na harakati za Rais Dkt. John Magufuli za kupambana na wizi wa mchanga wa dhahabu ambao jana amepokea ripoti ya suala hilo.
Kupitia mtandao wa kijamii Nikki ameandika, ‘Watanzania wanaopewa dhamana, wasipoamua kuwa waadilifu, umaskini utaandika historia tukufu kwa Tanzania, alafu kuna uhusiano gani kati ya uwekezaji na ufisadi…. maana kila kasha, wizi mkubwa utamkuta mwekezaji na wakala wake wa kitanzania (wasomi, viongozi, wafanya biashara), yaani ni kama ule uchumi wa kikoloni manufaa ni kwa makampuni ya nje na kitabaka cha watanzania wachache.
“Nimpongeze mkuu wa nchi kwa kuamua kupambana na ufisadi huu, ila vita ya kuvunja mfumo wa kiuchumi wa kifisadi ni hatari, kina Lumumba, Nkruma, Sankara, huko Chile, Nikaragwa, Venezuela, haiti, Iran…. viongozi hawakupona, ni vita kuu. Mungu akusimamie,” ameandika Nikki.