SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 11 Machi 2017

T media news

Umeisikia Hii ya Papa Francis Kuruhusu Wanaume Walio na Wake Kuwa Mapadri?

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis amesema kuwa huenda wakabadili sheria kuwaruhusu wanaume waliooa kuwa mapdri wa kanisa hilo.

Papa Francis alisema hayo akifanya mahojiano na gazeti moja la nchini Ujerumani ambapo alieleza kuwa, ni wakati sasa wa kufikiria jambo hilo kutokana na kanisa kukumbwa na uhaba wa mapadri hasa maeneo ya vijijini katika maeneo mbalimbali duniani.

Kiongozi huyo wa kanisa alisema, yeye yupo tayari kufanya mabadiliko hayo ambayo yataruhusu wanaume waliooa kubarikiwa na kuwa mapadri, lakini kwa wale ambao tayari ni mapadri, hawataruhusiwa kuoa.

Kanisa katoliki tayari limeruhusu baadhi ya watu waliooa kuwa watumishi kanisani. Wakristo ambao tayari wameoa kisha wakabadili dhehebu na kuwa wakatoliki wanaruhusiwa kuendelea kuwa kwenye ndoa na kuwa mapadri wa kanisa Katoliki kama watapa ridhaa kutoka kwa wake zao.

Kanisa Katoliki linaamini kuwa Padri hatakiwi kuoa kulingana na maandiko matakatifu katika biblia, na kwavile inaaminiwa kwamba Padri anatakiwa kuishi kama Kristo, na hivyo hatakiwi kuoa kama ilivyokuwa kwa Kristo Yesu.