SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 11 Machi 2017

T media news

Samatta amesema jina lake kwenye kikosi cha Europa litatoa fursa kwa wachezaji wa Bongo

UEFA wametoa kikosi bora cha wiki huku jina la Mtanzania Mbwana Samatta anayecheza klabu ya Genk ya Ubelgiji likiwa ni miongoni mwa wachezaji wanaounda kikosi hicho cha wiki.

Samatta ambaye ni nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ amesema, jina lake kuwa miongoni mwa wachezaji 11 wanaounda kikosi cha wiki cha Europa League, huenda kukafungua njia kwa wachezaji wengine wa kitanzania kuonekana zaidi kimataifa.

“Hata mawakala watapata hamu ya kujua Tanzania kuna vipaji vya aina gani, kwamba huyu yupo hapa ngoja tuangalie wengine kutoka kwao wakoje kwa sababu mimi siishi pekeangu Tanzania wapo wengine ambao bado haujafika muda wa wao kuonekana kwa kiasi kikubwa.”

“Kwa hiyo bendera inavyokuwepo pale nafikiri hata mawakala wanafikiri lazima kutakuwa na wengine wenye uwezo lakini hawaonekani, hivyo inatengeneza njia kwa wachezaji wengine wa kitanzania kuweza kusogea.”

“Haya ni mashindano makubwa na yana timu nyingi zenye wachezaji wengi wenye majina makubwa, kwangu kutokea kwenye kikosi cha UEFA ni kitu muhimu ambacho kinatengeneza mazingira mazuri ya baadae kwa sababu watu wanaanza kujiuliza huyu ni nani, kwa hiyo inatengeneza mazingira ya watu kukufatilia.”

“Kwangu ni kitu muhimu sana ukilinganisha na kiwango kilivyokuwa kwenye ile gamenafikiri watu wengi watakuwa wanatamani kujua huyu ni nani na kujaribu kufatilia nilipotokea na mambo mengi kuhusu career yangu na kunitupia jicho zaidi. Sio kila mchezaji anaweza kuingia kwenye kikosi cha wiki, inategemea na nini ulichofanya kwenye hiyo wiki.”

“Nadhani jambo hili ni muhimu kwangu na inatengeneza mazingira ya mimi kutoka hapa na kwenda mbele zaidi.”

Samatta amesema jambo jingine kubwa analolifurahia ni kuwa kwenye kikosi cha wiki cha Europa League pamoja na kiungo wa Manchester United Henrikh Mkhitaryan.

“Mimi ni mpenzi wa Manchester United, kwa hiyo moja kwa moja atakuwa ni Henrikh Mekhitarian. Ninapojikuta nipo na mchezaji wa Manchester, najisikia furaha kwa sababu inaleta picha ambayo hakuna mtu aliyekuwa anaifikiria kwamba kwenye kile kikosi kuna bendera ya Tanzania pia kwangu ni kitu ambacho najivunia.”