SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 9 Machi 2017

T media news

Profesa Ndalichako Afanya Usafi Ocean Road, Atoa Misaada..!!!!


Katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amefanya usafi na kutoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya Sh 4.5 milioni katika Taasisi ya Satarani ya Ocean Road.

Misaada iliyokabidhiwa jana asubuhi ni pamoja na kanga, sabuni za kuogea na kufulia, dawa za meno, juisi, maji ya kunywa, pampers na mabeseni.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo, Profesa Ndalichako alisema katika kusherehekea wanawake wa Mkoa wa Dar es Salaam kupitia Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) waliadhimia kuwatembelea wanawake wanaotibiwa saratani.

“Tunatambua kwamba wana mahitaji pia, kama ilivyo wanawake ndiyo nguzo ya maendeleo kwa hiyo anavyougua kwa muda mfupi familia hutetereka, tumekuja hapa na vifaa mbalimbali ambavyo tunaamini hawa wagonjwa wanavihitaji,” amesema Profesa Ndalichako.