SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 13 Machi 2017

T media news

Jeshi la Polisi Dar Wakusanya Milioni 840 za Faini Ndani ya Wiki Moja Tu...!!!!


Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam limefanikiwa kukusanya jumla ya shilingi milioni 840 za faini ya makosa mbalimbali ya barabarani kwa kipindi cha wiki moja ya oparesheni iliyofanywa na jeshi hilo.

Akiongea na waandishi wa habari Ijumaa hii, Kamishna wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema kiwango cha mapato hayo ni kidogo na inaashiria kupungua kwa makosa yanayofanywa na madereva.

“Kwa upande wa barabarani tunakwenda vizuri kati ya tarehe 1 mwezi 3 mwaka 2017 mpaka tarehe 9 mwezi wa 3 mwaka 2017 takribani siku hizo 8 tumeweza kukusanya jumla ya shilingi milioni 840 kwahiyo niseme tu kwamba mapato yanapungua hii tu ni kwasababu watu wameanza kutii tu sheria ya usalama barabarani,” Alisema Kamanda Sirro.