SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 14 Machi 2017

T media news

Exclusive: Harmonize Ataja Sababu za Kutoendana na Wolper, Azungumzia Umaarufu wa Harmorapa...!!!!!


MSANII wa kwanza kusainiwa kwenye Lebo ya Muziki ya WCB inayomilikiwa na Diamond Platinumz, Harmonize kwa mara ya kwanza amefunguka akitaja sababu ambazo wadau na mashabiki wamekuwa wakinong’ona kuwa haendani na mpenzi wake wanaedaiwa kuachana, msanii wa Bongo Movie, Jacqueline Wolper.

Akipiga stori na Global TV Online, juzi Jumamosi kwenye studio za WCB zilizopo Sinza Mapambano, Dar, Harmonize alisema:

“Kwanza namshukuru Mungu kwa mafanikio niliyoyapa mpaka sasa, nawashukuru menejimenti yangu kwa kunitengeneza mpaka kuwa Harmonize huyu anaeonekana leo.

“Ni mafanikio mengi nimeyapata ndani ya mwaka mmoja ikiwa ni pamoja na kushinda tuzo tatu za kimataifa.

“Watu wamekuwa wakisema hatuendani mimi na Wolper huenda kwa sababu yeye alianza kuwa staa kabla yangu wakati huo nikiwa kijijini au hatuendani kwa kuwa yeye anapesa nyingi pengine kuliko mimi!” alisema Harmonize.

Kuhusu Project zake Harmonize alisema.

“Nimetengeneza ngoma nyingi sana huenda ningeweza kuziachia kila mwezi lakini lazima tupeane  mimi na wasanii wenzangu wa WCB. (Rich Mavoko, Queen Darlin na Rayvany).

Kuhusu kumfahamu Harmorapa na kazi zake?

“Mara ya kwanza nilipomsikia, nilijiskia vibaya sana, nilikutana nae maisha klabu akawa analia iliniuma sana. Nachoweza kusema, ajitahidi na mimi namuombea aendeleea kukomaa atafanikiwa ili siku moja aisaidie familia yake” alisema Harmnize