SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 8 Machi 2017

T media news

Barnaba Afunguka Juu ya Kumfunika Diamond Kwa Show za Nnje ya Nchi..!!!


Muimbaji wa muziki Barnaba, amedai hana mpango wa kufanya kolabo na msanii wa nje kwa sasa kwa kuwa bado anajipanga vizuri kisanaa huku akidai yeye ni mwanamuziki anayeongoza kwa kufanya show nyingi za nje ya nchi.

Alisema si kwamba anaogopa ila kwa upande wake anaona bado anahitaji kujipanga zaidi ili atakapoamua kufanya kolabo yoyote iwe kubwa kama alivyorekodi na msanii wa Uganda, Jose Chameleone.

“Muziki hautaki kubahatisha, mimi ni mwanamuziki ninayeongoza kwa kufanya shoo nyingi nje ya nchi, lakini sijataka kumshirikisha msanii yeyote wa nje kwa kuwa muziki wangu bado nauandaa, unaenda kidogo kidogo na nikiona umefika ninakotaka nitafanya hivyo,” Barnaba aliliambia gazeti la Mtanzania.

Alisema kufanya hivyo hakumaanishi yeye ni msanii mdogo, ila katika maisha kila kitu lazima ufanye kwa malengo na baada ya wimbo wa ‘Love boy’ anatarajia kuachia wimbo wake mpya wa ‘Alone’