SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 14 Machi 2017

T media news

Baada ya Mkutano wa CCM Kuisha,Magufuli na Dk Shein Wameibuka na Hili Jipya...!!!


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli Jumatatu hii amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma.

Taarifa iliyotolewa na Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Ikulu,Jaffar Haniu imesema:

Rais Magufuli amesema katika mazungumzo yao wamezungumza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kumtakia heri Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein kufuatia leo kuwa siku yake ya kuzaliwa

Kwa upande wake Rais Dkt. Ali Mohamed Shein amesema anamshukuru Rais Dkt.Magufuli kwa kumtakia heri katika siku yake muhimu ya kuzaliwa na hivyo wamekutana kubadilishana mawazo katika kuhakikisha wanajenga nchi na kusonga mbele.

“Siku ya kuzaliwa ni siku ya furaha lazima ikumbukwe lazima isherehekewe, mimi siku yangu ya kuzaliwa sisherehekei sana lakini huwa nafurahi sana na leo nimefurahi sana” amesema Dkt. Shein.

Dkt.Shein amesema ametumia siku yake ya kuzaliwa kumtembelea Rais Dkt.Magufuli ili waweze kubadilishana mawazo kwani wana kazi kubwa ya kujenga nchi.