SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 22 Februari 2017

T media news

Wenye Simba yenu, mmeyasikia maneno ya Jini Kabula?

PAMBANO la watani wa jadi Simba na Yanga limekuwa likivuta hisia za watu wengi sana toka ndani na nje ya nchi tangu miamba hiyo ilivyoanzishwa kutokana na ushindani uliopo baina ya timu hizo.

Muigizaji nyota wa Bongo Movies Miriam Jolwa  maarufu kama ‘Jini Kabula’ ambaye ni shabiki wa damu wa timu ya Yanga ametamba kikosi chake kitaibuka na ushindi kwenye mchezo wao utakaopigwa Febuari 25 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kutokana na uimara wa kikosi chao ukilinganisha na wapinzani wao Simba.

Jini Kabula aliyetamba sana katika tamthiliya ya ‘Jumba la dhahabu’ iliyoandaliwa na muongozaji Tuesday Kihangala na kurushwa na Shirika la utangazaji la Tanzania (TBC 1) amesema kwa sasa hakuna timu ya kuisumbua Yanga kwa msimu huu.

Shaffidauda.com.tz ilizungumza na Kabula ambaye amesema, kuwa anakiamini kikosi chake kwakua kipo kwenye ubora mkubwa huku wakiwa mabingwa watetezi kwahiyo amewahakikishia Watani wao kuwa kichapo kipo pale pale.

“Sisi mashabiki wa Yanga hatuna wasi wasi na timu yetu tunategemea kuibuka na ushindi mkubwa kama msimu uliopita na jeuri hiyo tunayo kwakua tuna kikosi imara kuliko Simba,” alisema Kabula ambaye ni mhudhuriaji mzuri wa mechi za Yanga.

Aidha muigizaji huyo amewataja washambuliaji Saimon Msuva na Amissi Tambwe kuwa ndiyo watu watakao peleka kilio kwa Wana Simba Jumamosi pale uwanja wa Taifa.

“Sijaona beki wa kuwazuia Msuva na Tambwe wasifunge kwenye kikosi cha Simba, nawaomba watani wakae mkao wa kuumizwa wikiendi hii,” alimaliza Kabula.