SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 22 Februari 2017

T media news

MSANII MADEE AZITOLEA POVU MEDIA ZINAZO PROMOTE WATU KAMA HARMORAPA

Ni ukweli usiofiichika kwamba Harmorapa ni mmoja kati ya watu ambao wamebeba vichwa vingi vya habari toka mwishoni mwa mwaka jana mpaka mwaka huu umeanza na sasa ni mwishoni mwa mwezi wa pili.

Ikiwaimebeba maana tosha kwamba rapper huyo amejizolea umaarufu mkubwa sana kutokana na kuzungumziwa mara kwa mara katika mitandao ya kijamii kitu ambacho kimezipelekea media mbali mbali kumpatia interviews na vitu kama hivyo.

Sasa raisi wa Manzese Madee amelaani vikali vitendo hivyo vya media kumpa nafasi mtu kama Harmorapa na hatimaye kumpa jina kurahisi rahisi namna hiyo wakati kuna wasanii wana vipaji ila wanakosa vitu kama hivyo ili kukuza muziki wao na vitu kama hivyo.

Akiongea na Perfect255 Madee amefunguka kuwa huo ndio ujinga ambao kila siku huwa anaupinga, yani vyombo vya habari kupoteza time kwa watu ambao wanaonekana kabisa wanalazimisha vitu.

“Ni upumbavu kupoteza muda kumpa interviews mtu kama huyo, kumuacha aandikwe kwenye vyombo vya habari. Hivyo vitu tungewatafuta watu wenye vipaji vya ukweli mitaani tukawapa promo kama hiyo naamini tungekuwa na wanamuziki wengi wazuri lakini hivi sasa vitu vya kijinga ndio vinapewa sana nguvu, vitu ambavyo sio vya kijinga vinafinywa. Sio kitu kizuri, mimi sipendi wala nini.” Alisema Madee.